Na Mkunde Mathias Moshi.
Moshi, Mkuu wa wilaya ya same, Mkoani Kilimanjaro Edward Mpogolo, Amesema mkoa wa Kilimanjaro ni miongoni mwa mikoa hapa nchini wanawake waishio vijijini wanakabiliwa na changamoto ya umilikiwa ardhi.
Akizungumza wakati akipokea matembezi ya wanawake wakitokea mkoa wa mwanza wakihamasisha wanawake wa vijijini kumiliki ardhi yaliyoanzia mkoa wa mwanza na hitimisho yatakuwa mkoa wa Kilimanjaro kuadhumisha siku ya mwanamke vijijini duniani.
Mpogolo aliwapongeza mashirika yote yaliyojitoa kufadhili matembezi ya kutetea wanawake wa vijijini kuwa na uwezo wa ardhipamoja na kukabiliana na changamoto zinazowakabili.
Alisema miomngoni mwa mikoa yenyechangamoto ya wananwake kumiliki ardhi ni pamoja na mkoa wa Kilimanjaro hivyo madhimisho kufanyika hapa ni sahihi kabisa.
“Mwanamke akifa mwanaume anamiliki ardhi bila shida yoyote lakini mwanaume akitanguli migogoro ya umiliki wa ardhi hiyo hiyo inaibuka ambapo ndugu wa mwanaume wanataka kumiliki ardhi hiyo hali chambo sio sawa kabisa”amesema.
Waandaji wa msafara, Mussa Masongo, amesema msafara ulianzia Mwanza , ukapita Misungwi, Babati, na Arusha na hitimisho ni hapa Kilimanjaro, ambapo amesema msafara umejenga kutoa elimu kwa wanajamii na taifa kwa ujumla
Amesema , Misungwi kumeonekana kuwepo kwa swala la upimaji na urasilimishaji wa ardhi kwa mwanamke bado ni tatizo, huku Babati kukiwa matukio ya ukatikli kwa wananwake badi ni changamoto, na Arusha kumeonekana migogoro ya ardhi bado ni tatazo.
Amesema Malengo ya serikali yamlenga kumwezesha mwanamke wa kijijini kwa kuboresha huduma za kimaendeleo maeneo ambayo hayo kwa kuwafikishia huduma zote .
“tulioko mjini tunazaa lakini watoto wanapelekwa vijijini ambapo wanalelea na bibi ambae ni mwanamke , anabebeshwa mizigo mamboa wazazi mtoto huyo wapo mijijini hii dhana pia ni ya kukemea ili kumkomboa mwanamke wa kijijini”
iongozi wa Msafara Afisa Maendeleo Mkoa wa Mwanza, Janeth Shishira, amesema Serikali na wadau imeona umuhimu wa mwananamke vijiji , kuona nama ya kuboredha siku ya manamke wa vijijini, katika kuboresha na kuona umuhimu wao, kwa kuwafikishia huduma karibu.
“lengo la matembezi haya ni Kuhamasisha wanawaka kufahamu haki zao katika umiliki wa ardhi haswa wale wa vijijini’ amesema
Aidha amesema matembezi hayo yameenda sambamba na kuhamasisha wanawake kuchukua uviko 19 kama fursa na kwenda kuchanja ili kujikiga na maambukizi ya uginjwa huo badala ya kuona ni changamoto.
Maadhisho ya siku ya mwanamke wa vijijini yataadhimishwa oktoba 15,2020 katika viwanja vya pasua Mandela ambayo yataenda samabamba na matukio mbalimbali ya mbio za riadha za kilomita 5,10,21 na kongamano la simulizi mbalimbali kuhusu mwanamke wa vijijini na changamoto zinzaomkabili