Mwenyekiti Tume ya haki za Binaadamu na Utawala bora Mathew Mwaimu akiwakaribisha Masheha wa Shehia mbali mbali za Wilaya ya magharibi “A” na “B” katika mafunzo yanayohusu haki za Binaada na Utawala bora yaliyoandaliwa na Tume ya haki za Binaadamu na Utawala Bora Tanzania yaliyofanyika Ukumbi wa Maleria Mwanakwerekwe Zanzibar.
Afisa Uchunguzi Mkuu Tume ya Haki za Binaadamu na Utawala Bora Upande wa Zanzibar Hussein Kh. Mbarouk akiwasilisha mada ya wajibu wa kamati za Shehia katika kupambana na vitendo vya ukatili na udhalilishaji kwa Wanawake na watoto katika mafunzo ya masheha kuhusu haki za binaadamu yaliyofanyika Ukumbi wa Maleria Mwanakwerekwe Zanzibar.
Sheha wa Shehia ya Chuini Mohammed Sheha Kheir akichangia mada katika mafunzo ya Haki za Binaadamu na Utawala bora yaliyofanyika Ukumbi wa Maleria Mwanakwerekwe Zanzibar.
Mwanasheria katika Tume ya Haki za Binaadamu na Utawala Bora kwa upande wa Zanzibar Wilfred Msagati akiwasilisha mada kuhusu ulinzi wa haki za wanawake na watoto katika mafunzo yanayohusu haki za Binaadamu kwa Masheha wa Shehia za Wilaya ya Maghribi “A’ na “B” huko Ukumbi wa Maleria Mwanakwerekwe Zanzibar.
Sheha wa Shehia ya Mwanakwerekwe Amani Ayoub Makame akichangia mada katika mafunzo ya Haki za Binaadamu na Utawala bora yaliyofanyika Ukumbi wa Maleria Mwanakwerekwe Zanzibar.
Kamishna Tume ya Haki za Binaadamu na Utawala Bora Amina Talib Ali akichangia mada katika mafunzo ya Haki za Binaadamu na Utawala bora yaliyofanyika Ukumbi wa Maleria Mwanakwerekwe Zanzibar.
Mratibu wa jinsia Tume ya Haki za Binaadamu na Utawala Bora Dodoma Florence Chaki akiwasilisha mada kuhusu hali ya ukatili na udhalilishaji kwa wanawake na watoto Zanzibar katika mafunzo yanayohusu haki za Binaadamu kwa Masheha wa Shehia za Wilaya ya Maghribi “A’ na “B” yaliyofanyika Ukumbi wa Maleria Mwanakwerekwe Zanzibar.
Sheha wa Shehia ya Kibweni Subira Haji Yahya akichangia mada katika mafunzo ya Haki za Binaadamu na Utawala bora yaliyofanyika Ukumbi wa Maleria Mwanakwerekwe Zanzibar.
Sheha wa Shehia yam Mnarani Ramadhan Abdalla Rajab akichangia mada katika mafunzo ya Haki za Binaadamu na Utawala bora yaliyofanyika Ukumbi wa Maleria Mwanakwerekwe Zanzibar.
PICHA NA FAUZIA MUSSA –MAELEZO ZANZIBAR.
…………………………………………………………………..
Na Khadija Khamis ,Maelezo Zanzibar
Mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binaadamu na Utawala Bora Mathew P.M.Mwaimu amewataka Masheha kulitafutia ufumbuzi tatizo la ukatili na udhalilishaji wa kijinsia dhidi ya wanawake na watoto kwa njia ya kutoa elimu katika jamii .
Hayo ameyasema leo katika Ukumbi wa Malaria Mwanakwerekwe wakati akitoa mafunzo ya haki za binaadamu na utawala bora kwa Masheha wa Shehia mbali mbali za Wilaya ya Magharibi “A” na “B”.
Alisema suala zima la utoaji wa elimu kwa jamii iwe ndio agenda ya kudumu na kuhakikisha athari za ukiukwaji wa misingi ya utawala bora zinaondoshwa .
Aidha amesema Tume ya Haki za Binaadamu na Utawala Bora inatambua na kupongeza juhudi mbali mbali zinazofanywa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na wadau mbali mbali za kulinda na kukuza haki za wanawake na watoto pamoja na kulitafutia ufumbuzi tatizo la ukatili na udhalilishaji wa kijinsia.
Ameeleza kuwa pamoja na hatua hizo na mikakati mbali mbali ya kukabiliana na ukatili huo, bado suala la rushwa limepungua kwa kiwango kidogo sana hivyo mikakati madhubuti zaidi inahitajika kukabiliana na tatizo hilo.
Alifahamisha kuwa kazi ya Tume hiyo ni kutoa ushauri kwa Serikali katika changamoto mbali mbali ili ziweze kupatiwa ufumbuzi unaostahiki kwa mujibu wa sheria .
Nae Mkurugenzi Msaidizi wa Tume ya Haki za Binaadamu na Utawala Bora, Fides Shao akitoa mada ya Ukatili alisema ni kitendo chochote kinachofanywa kwa mtu na kusababisha madhara ya kimwili na kiakili au mateso kwa wanajamii ikiwa kwa kutishiwa maisha pamoja na kunjimwa uhuru wa hadharani au kificho .
“kitendo hicho kinachangia kukosesha ushirikiano katika jamii hasa wakati wa kutoa ushahidi katika kesi za ukatili na udhalilishaji, “alisema Mkurugenzi huyo .
Nao Masheha hao walisema wanasikitishwa na baadhi ya kesi zinazowafikia ambazo zinaushahidi wa kutosha na kukanushwa kukosa ushahidi katika hatua za mwisho.
Walisema kuwa suala la rushwa na muhali bado ni tatizo katika jamii jambo ambalo linazorotesha mfumo sahihi wa kutoa taarifa na kudai haki .