Mkuu wa Wilaya ya Ulanafa,Mhe Ngollo Malenya akizungumza mbele ya waandishi wa habari hawapo pichani kuhusu uwepo wa Tamasha la kuhamasisha awekezaji katika Wilaya ya Ulanga litakalofanyika Oktoba 22 na 23 katika Uwanja wa Mapinduzi uliopo Mjini Mahenge,
Mmoja wa Waratibu wa tamasha linalotarajia kufanyika Wilayani Ulanga .Michael
Lyachema akifafanua baadhi ya mambo mbalimbali kuhusiana na tamasha
hilo la kuhamasisha wawekezaji katika Wilaya ya Ulanga litakalofanyika
Oktoba 22 na 23 katika Uwanja wa Mapinduzi uliopo Mjini Mahenge.
Waandishi wa Habari wakimsikiliza Mkuu wa Wilaya ya Ulanga Mhe.Ngollo Malenya alipkuwa akizungumza nao leo jijini Dar
………………………………….
SERIKALI Wilayani Ulanga, Morogoro imetaja fursa tisa zinazopatikana katika
Wilaya hiyo ambapo imetoa wito kwa watanzania kuzichangamkia katika
kuwekeza na kufanya biashara.
Mwito huo umetolewa leo na Mkuu wa Wilaya hiyo, Ngollo Malenya wakati
akizungumza na wandishi wa habari kuhusu uwepo wa Tamasha la kuhamasisha
wawekezaji katika Wilaya ya Ulanga litakalofanyika Oktoba 22 na 23
katika Uwanja wa Mapinduzi uliopo Mjini Mahenge.
DC Malenya amesema lengo la tamasha hilo ni kutangaza fursa zilizopo
wilayani humo pamoja na kuunga mkono juhudi za Rais Samia Suluhu Hassan
katika kuitangaza na kukuza pato la Taifa.
“Lengo la Tamasha hili la kuhamasisha uwekezaji katika Wilaya ya Ulanga
linajulikana kama ULANGA IHEREPA, yaani AMAZING ULANGA, ULANGA
KUNAPENDEZA, neno” Iherepa” lina maana inapendeza kwa lugha ya wenyeji
wa Wilaya ya Ulanga WAPOGORO. Kauli mbiu ya Tamasha hili ni ‘‘TWENZETU
ULANGA’’ Amesema DC Malenya
DC Malenya amesema pamoja na mambo mengine ya uwekezaji wanatarajia kuwa
na michezo mbalimbali kama vile Riadha, kupanda milima (Hiking), Mbio za baiskeli (Mountain biking) pamoja na Ngoma za asili.
Aidha wageni kutoka ndani na nje ya nchi watapata fursa ya kutembelea maeneo
ya vivutio ikiwa ni pamoja na utalii wa mazingira ya asilii, utalii wa
majengo ya kihistoria, utalii wa hifadhi za misitu pamoja na kufanya
utalii wa kuvua samaki.
Amezitaja fursa zilizopo katika Wilaya hiyo kuwa ni fursa katika sekta ya Madini,
sekta ya kilimo na ufugaji, uzalishaji wa asali, utalii, uvuvi, ngoma
za asili na majengo ya kihistoria.
”
Wilaya yetu ina fursa za uwekezaji katika tafiti za madini, uchimbaji
wa madini, ubia na wamiliki wa leseni za maeneo ya madini ambao wana
leseni lakini hawana mitaji, vifaa na teknolojia ya uchimbaji wa madini.
Aina ya madini yanayopatikana Wilayani Ulanga ni pamoja na Madini ya
Kinywe (Graphites), Rubi na Dhahabu.
Wilaya ya Ulanga ina eneo lenye ukubwa wa hekta 1,068,889.43 ambapo kati ya
hekta hizo ni hekta 269,775.34 ambazo sawa na 23.95% zinafaa kwa
shughuli za kilimo na hekta 11,714 zinatumika kwa kilimo cha
umwagiliaji,” Amesema DC Malenya