“Kuundwe kamati zitakazosimamia lakini kumeshaonekana kuna fedha hapa,kutakuwa na utitiri wa kamati..sitaki utitiri wa kamati,kuundwe kamati za wataalamu katika ngazi za mikoa watakaosimamia hadi ngazi za wilaya chochote kitakachotokea wilayani tunakamata kamati ya mkoa ambayo inasimamia miradi hiyo hapo ndio tunaweza kuwa na Responsibility inayoeleweka,tukisema nani kampasia nani hatutaweza kushika mtu lakini kamati zikiwa ndogo tunaweza kushika mtu”
“Nikuagize Waziri Mkuu kwenye ile kamati ya kitaifa uongoze kamati hiyo na msimamie mpango mzima huu wa Mradi huu wa Maendeleo kwa Wananchi”
“Jambo lingine ni kwa Viongozi,Watumishi na Wazabuni…hili niliseme tu kwa wale wanaotaka kuzijua rangi zangu halisi …mkinitizama hivi mnasema Mhe.Rais ni mweupe lakini nina rangi halisi,kwa wale wanaotaka kuzijua rangi zangu halisi wajaribu kudokoa fedha hizi au wabadilishe matumizi ya fedha hizi bila maelewano”
“Ukiangalia programme hii,Nchi inakwenda kuchemka,kila kona inakwenda kuwa na ujenzi inakwenda kuwa na Miradi ya Maendeleo,niwatake Wakurugenzi wa Halmashauri na timu zao kule chini kwenda kuisimamia Miradi hii ipasavyo”
“Kwenye fedha hii sina huruma na mtu kwasababu,nina uwezo wa kupata mikopo mengine yenye gharama nafuu ambayo itaweza kutusogeza kwa haraka,tukivurunda hapa tayari tutakuwa tumejitia doa,kwahiyo sitakuwa na huruma na mtu atakayekwenda kuichezea fedha hii kuanzia Mawaziri wangu,chini kwa Wakurugenzi na wanaowafuata”
Ameyasema Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Samia Suluhu Hassan wakati wa Uzinduzi wa kampeni ya Maendeleo kwa Ustawi wa Taifa na Mapambano dhidi ya UVIKO – 19,Leo Oktoba 10,2021 Katika Ukumbi wa JKCC Jijini Dodoma.