Posta Mkoa wa Singida Mary
Kimaro akieleza mpangilio wa matukio yatakayofanyika kwenye Maadhimisho ya Siku ya Posta
Duniani Oktoba 9 mwaka huu kwa Mkoa wa Singida.
Wafanyakazi wa Shirika la Posta Mkoa wa Singida wakiwa na furaha kwenye maadhimisho mbalimbali yanayoendelea kuelekea kilele
cha Siku ya Posta Dunia Oktoba 9 mwaka huu.
Maadhimisho hayo kimkoa yanatarajiwa kufanyika kwenye Shule ya Sekondari Singitu iliyopoTarafa ya Mtinko,
Wilaya ya Singida mkoani hapa.
la uandishi wa barua lililotangazwa na shirika hilo kuelekea kilele.
la Posta Singida.
cha
maadhimisho hayo kama sehemu ya shirika hilo kuunga mkono juhudi za serikali dhidi ya mapambano ya ugonjwa huo .
la Posta mkoani Singida kwa wateja mbalimbali kuelekea kilele cha Maadhimisho ya Siku ya
Posta Duniani kwa mwaka huu.
cha Siku ya Posta Duniani ndani ya ofisi Ya shirika hilo kwa mkoa wa Singida
Na Godwin
Myovela, Singida
SHEREHE za Siku
ya Posta Duniani ambazo hufanyika kila ifikapo Oktoba 9 ya kila mwaka kwa Mkoa wa
Singida mwaka huu zinatarajiwa kuadhimishwa kwenye shule ya Sekondari Singitu iliyopo
Tarafa ya Mtinko Wilaya ya Singida mkoani
hapa.
Imeelezwa sababu
ya kufanyika shuleni hapo ni kutokana na shule hiyo kuibuka kinara kwa kutoa idadi
kubwa ya wanafunzi waliojitokeza kushiriki shindano la uandishi wa barua katika
kuelekea kilele cha maadhimisho ya siku ya Posta mwaka huu.
Sambamba na hilo,
katika maadhimisho hayo timu ya wafanyakazi wa shirika hilo itaambatana na jopo
la wataalamu wa afya ambao pamoja na mambo mengine watajikita katika kutoa elimu
juu ya ugonjwa wa COVID 19 zoezi ambalo litakwenda sanjari na ugawaji wa vifaa mbalimbali
vya kujikinga, ikiwa ni sehemu ya shirika hilo kuunga mkono jitihada mbalimbali
zinazofanywa na serikali katika mapambano dhidi ya ugonjwa huo.
Akizungumza na
vyombo vya habari ofisini kwake, Kaimu Meneja wa Posta Mkoa wa Singida, Mary
Kimaro alisema pia maadhimisho ya mwaka huu yenye kaulimbiu isemayo ‘Ubunifu kwa
Posta Endelevu’ ambayo kitaifa yanatarajia kufanyika jijini Dodoma, shirika hilo
pamoja na mambo mengine litajikita zaidi katika kujitangaza na kueleza umma juu
ya maboresho yake makubwa ya kihuduma yanayoendelea kutolewa kwa sasa kwa kuzingatia
mifumo ya kidijitali ikilinganishwa na siku za nyuma.
“Lengo hasa
la kuadhimisha kwenye shule hii ni kuongeza hamasa kwa shule na washiriki wengine
kuiga mfano huo na kufanya vizuri zaidi kwenye maadhimisho ya mwaka utakao fuata…Posta
kwa sasa tupo kidijitali zaidi nitoe wito kwa umma kuzidi kutembelea ofisi za shirika
letu na kutuunga mkono kwa kujipatia huduma zetu mbalimbali za kidijitali zilizoboreshwa.”
Alisema Kimaro.
Shirika hilo
kwa sasa pamoja na mambo mengine linatoa huduma za kidijitali za Duka Mtandao,
Intaneti Café, tuna mfumo madhubuti wa kufuatilia barua au kifurushi kilichotumwa
kupitia mtandao kujua kimefikia wapi au kimepokelewa na nani.
Pia Kimaro alieleza
kuwa Posta ndani ya Singida kwa kuzingatia mifumo ya kasi ya TEHAMA linaendelea
kusafirisha barua kwa njia ya haraka (EMS) ndani na nje ya nchi, usafirishaji mizigo
mikubwa, kutoa huduma ya masanduku ya barua ikiwemo kwa kutumia TEHAMA ya Posta
Kiganjani na huduma ya Uwakala wa Fedha.
Pia kwa mujibu
wa Kaimu huyo Meneja shirika hilo pia lina magari ya uhakika kwa usafirishaji wa
vifurushi vya hadi tani 30 hivyo watanzania wanakumbushwa kuchangamkia fursa hiyo
ya usafirishaji mizigo kwa njia ya magari
kwa mikoa ya Dar es Salaam, Mwanza na Kigoma kwa kuingia na kutoka Singida kila
siku kuanzia majira ya saa 10 jioni.
“Magari yetu
ya Dar es Salaam hupitia miji ya Morogoro, Dodoma na Manyoni, na yale ya Mwanza
hupitia njia ya Shinyanga huku yale ya Kigoma hupitia miji ya Nzega, Tabora,
Urambo hadi Kigoma,”alisema Kimaro.
Tangu kuanzishwa
kwake kwa Sheria ya Bunge Namba 19 ya Mwaka 1993 nakuanza kazi rasmi Januari Mosi,
1994 shirika hilo hatua kwa hatua limeendelea kufanya maboresho makubwa katika utoaji
wa huduma zake mbalimbali, zikiwemo huduma ya usafirishaji wa fedha kwa njia ya
‘Posta Cash’, Uwakala wa Bima, Huduma za uuzaji wa hisa za makampuni mbalimbali
na huduma za Bodi ya Mikopo na Baraza la Mitihani.