Mkuu wa wilaya wa Dodoma,Jabir Shekimweri,akizungumza katika Mkutano wa wazi na walimu wa wilaya ya Dodoma wa kujadili masuala mbalimbali ya Maendeleo ya Mwalimu na ustawi wa Taifa uliofanyika katika uwanja wa Jamhuri Dodoma.
Mganga Mkuu wa wilaya ya Dodoma,Andrew Medhed,akitoa elimu ya Uviko-19 kwa walimu wa wilaya ya Dodoma mjini wakati wa Mkutano wa wazi wa kujadili masuala mbalimbali ya Maendeleo ya Mwalimu na ustawi wa Taifa uliofanyika katika uwanja wa Jamhuri Dodoma.
Baadhi ya walimu wakifatilia hotuba ya Mkuu wa wilaya wa Dodoma,Jabir Shekimweri,(hayupo pichani) wakati wa Mkutano wa wazi na walimu wa wilaya ya Dodoma wa kujadili masuala mbalimbali ya Maendeleo ya Mwalimu na ustawi wa Taifa uliofanyika katika uwanja wa Jamhuri Dodoma.
……………………………………………………
Na.Erick Mungele,Dodoma
Mkuu wa wilaya wa Dodoma,Jabir Shekimweri,ametoa wito kwa walimu wa Dodoma kupata chanjo ya dhidi ya UVIKO-19 ili iweze kuwasaidia katika kujilinda pamoja na wanaowazunguku.
Hayo ameyasema jijini Dodoma wakati wa Mkutano wa wazi na walimu wa wilaya ya Dodoma wa kujadili masuala mbalimbali ya Maendeleo ya Mwalimu na ustawi wa Taifa.
Bw.Shekimweri,amewaomba kuchanja kwa hiari yao ili kufikisha elimu kwa jamii kupitia vikao vya wazazi kwani mkishachanja itakuwa rahisi kufikisha elimu kwa jamii kutokana nafasi waliopo.
Aidha amesema Halmashauri ya jiji na Mkoa katika ziara watakazofanya watashirikiana na walimu bega kwa bega na kuwapa kipaumbele pale watakapo hitaji msaada na sasa wapo kwenye mpango wa kuanda namna ya walimu kuwa waanada mitihani ya taaluma kwa pamoja.
“Natoa wito kwa nyinyi walimu kuchanja maana mnapita katika mizunguko mingi na wanawao wazunguna na mnafasi ya kufikisha elimu kwa jamii katika vikao vyenu hasa kwa wazazi na wanafunzi.
Kwa upande wake Mganga Mkuu wa wilaya ya Dodoma,Andrew Medhed,ametoa elimu juu ya chanjo ya Covid -19 na kuwahakikishia walimu hao chanjo ni salama na kuachana na fikira Potofu za Mitandaoni maana chanjo wametumia nchi tofauti na Magonjwa tofauti kama vile Polio na Surua.
“kwa sababu mshapata elimu juu ya chanjo mkawe nguzo kutoa elimu kwa jamii kuhusiana chanjo ya Covid -19 na ni salma lakini pia jamii inapaswa kuendelea kujikinga pamoja na kuchukua tahadhari kama wataalam wa afya wanavyoelekeza”amesema
Naye Mmoja ya washiriki wa kikao hicho,Mwalimu Kileo Richard,ametoa ushauri kwa Serikali kama itawezekana baadhi ya taasisi au sehemu yenye mizunguko ya watu kila siku kuwa ni lazima kuchajanja.