Na Kadama Malunde – Malunde 1 blog
Askofu Mkuu wa Kanisa la EAG (T) Dkt. Brown Abel Mwakipesile ameweka Wakfu Jengo la Kanisa la EAG (T) Ushirika Shinyanga ‘Makimbilio Healing Centre’ huku akiwataka waumini wa Kanisa hilo kutumia jingo hilo kwa ajili ya Ibada na sala na siyo vinginevyo.
Ibada ya kuweka Wakfu Jengo la Kanisa la EAG (T) Ushirika Shinyanga imefanyika leo Jumapili Oktoba 3,2021 ambapo Mgeni Rasmi alikuwa Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Dk. Philemon Sengati kwa niaba ya Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Philip Mpango.
Akitoa neno na maombi ya kuweka Wakfu Jengo la Kanisa la EAG (T) Ushirika Shinyanga, Askofu Mkuu wa Kanisa la EAG (T) Dkt. Brown Abel Mwakipesile amesema jengo hilo likawe nyumba ya sala na siyo vinginevyo.
“Jengo hili la Kanisa la EAG (T) Ushirika Shinyanga limejengwa kwa fedha za waumini. Sisi tunajitegemea, tumejenga kwa fedha zetu sisi wenyewe, hapa hakuna Mfadhili kutoka nje ya nchi. Hatukujenga kwa nguvu ya Wazungu”,amesema Askofu Mwakipesile.
“Kukamilika kwa ujenzi wa Kanisa hili kunatokana na maono makubwa na moyo wa pekee wa Askofu Raphael Machimu, asiyekata tamaa na jengo hili linafanya tuwe na makanisa zaidi ya makanisa 5000”,amesema.
Dkt. Mwakipesile ameishukuru Serikali kuendelea kutoa uhuru wa kuabudu bila ya kuwapo bhughuza yoyote ile na kuahidi kuendelea kuhubiri amani ya nchi ili kuwaletea maendeleo wananchi.
Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Dk. Philemon Sengati akizungumza kwa niaba ya Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Philip Mpango amezishukuru taasisi za dini kwa kuendelea kushirikiana na serikali katika kudumisha amani , utulivu na mshikamano nchini.
“Tunayashukuru madhehebu ya dini na dini zote kwa kuendelea kushirikiana na serikali katika kudumisha amani ya nchi lakini kwa shughuli mbalimbali mnazofanya kwa ajili ya maendeleo ya nchi”,amesema Dkt. Sengati.
“Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inayoongozwa na Rais wetu Mpendwa Mhe. Samia Suluhu Hassan inatambua kazi nzuri inayofanywa na taasisi za dini katika Nyanja zote za maendeleo”,ameongeza Sengati.
“Nipo Kanisani hapa kumwakilisha Makamu wa Rais Dk. Philip Mpango, ambaye yupo kwenye majukumu mengine ya kitaifa, anaomba viongozi wa Madhehebu ya kidini muendele kuhubiri amani ya nchi,” amesema Dkt. Sengati.
“Serikali tunatambua kazi ya viongozi wa dini, ambapo mnaimarisha misingi ya upendo, utu, uzalendo, na mshikamano kwa wananchi, na kuifanya Tanzania kuendelea kuwa na amani na utulivu,” amesema.
Dkt. Sengati, ametumia fursa hiyo kuwahamasisha Watanzania kujitokeza kwa wingi kupata Chanjo ya UVIKO-19 na kupuuza maneno ya upotoshaji juu Chanjo hiyo ili siku wakipata maambukizi ya virusi vya Corona wasipate madhara makubwa.
Mwenyekiti wa Kamati ya Ujenzi wa Jengo la Kanisa la EAG (T) Ushirika Shinyanga, John Ntalimbo amesema Kanisa hilo lilianzishwa mwaka 1993 likiwa na waumini wanne na mpaka sasa lina waumini 600.
“Ujenzi wa Jengo hili lililoanza kujengwa mwaka 2003 unatokana na maono ya Askofu Raphael Machimu. Tumefanikiwa kujenga Kanisa hili kwa sababu ya uongozi mzuri wa Askofu Machimu ambaye ametujenga katika matoleo, tumeendesha machangizo na michango mbalimbali kanisani”,amesema Ntalimbo.
Askofu wa Kanisa la Kanisa la EAG (T) Ushirika Shinyanga, Raphael Machimu amemshukuru Mwenyezi Mungu kwa kuwawezesha kujenga Kanisa hilo lililotokana na michango ya kawaida kutoka kwa watu wa kawaida kanisani wazalendo na wenye imani na moyo wa kujitoa bila kutegemea misaada kutoka kwa watu nje ya nchi.
Amesema Kanisa hilo ambalo amesema limetumia zaidi ya Shilingi milioni 800 mpaka sasa lina uwezo wa kubeba watu takribani 2500.
ANGALIA PICHA HAPA CHINI
Askofu Mkuu wa Kanisa la EAG (T) Dkt. Brown Abel Mwakipesile akiweka Wakfu Jengo la Kanisa la EAG (T) Ushirika Shinyanga ‘Makimbilio Healing Centre’ leo Jumapili Oktoba 3,2021. Picha na Kadama Malunde
Askofu Mkuu wa Kanisa la EAG (T) Dkt. Brown Abel Mwakipesile akitoa neno na maombi ya kuweka Wakfu Jengo la Kanisa la EAG (T) Ushirika Shinyanga ‘Makimbilio Healing Centre’.
Askofu Mkuu wa Kanisa la EAG (T) Dkt. Brown Abel Mwakipesile akiomba wakati akiweka Wakfu Jengo la Kanisa la EAG (T) Ushirika Shinyanga ‘Makimbilio Healing Centre’.
Askofu Mkuu wa Kanisa la EAG (T) Dkt. Brown Abel Mwakipesile akiweka Wakfu Jengo la Kanisa la EAG (T) Ushirika Shinyanga ‘Makimbilio Healing Centre’ leo Jumapili Oktoba 3,2021.
Askofu Mkuu wa Kanisa la EAG (T) Dkt. Brown Abel Mwakipesile akiweka Wakfu Jengo la Kanisa la EAG (T) Ushirika Shinyanga ‘Makimbilio Healing Centre’ leo Jumapili Oktoba 3,2021.
Waumini wakiwa kwenye Kanisa la EAG (T) Ushirika Shinyanga ‘Makimbilio Healing Centre’.
Muonekano wa Jengo la Kanisa la EAG (T) Ushirika Shinyanga ‘Makimbilio Healing Centre’.
Muonekano wa Jengo la Kanisa la EAG (T) Ushirika Shinyanga ‘Makimbilio Healing Centre’.
Muonekano wa Jengo la Kanisa la EAG (T) Ushirika Shinyanga ‘Makimbilio Healing Centre’.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Dkt. Philemon Sengati akizungumza katika Ibada ya kuweka Wakfu Jengo la Kanisa la EAG (T) Ushirika Shinyanga ‘Makimbilio Healing Centre’.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Dkt. Philemon Sengati akizungumza katika Ibada ya kuweka Wakfu Jengo la Kanisa la EAG (T) Ushirika Shinyanga ‘Makimbilio Healing Centre’.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Dkt. Philemon Sengati akizungumza katika Ibada ya kuweka Wakfu Jengo la Kanisa la EAG (T) Ushirika Shinyanga ‘Makimbilio Healing Centre’.
Mwenyekiti wa Kamati ya Ujenzi wa Jengo la Kanisa la EAG (T) Ushirika Shinyanga, John Ntalimbo akizungumza katika Ibada ya kuweka Wakfu Jengo la Kanisa la EAG (T) Ushirika Shinyanga ‘Makimbilio Healing Centre’.
Viongozi mbalimbali wa dini na serikali wakiwa kanisani.
Askofu wa Kanisa la Kanisa la EAG (T) Ushirika Shinyanga, Raphael Machimu akizungumza katika Ibada ya kuweka Wakfu Jengo la Kanisa la EAG (T) Ushirika Shinyanga ‘Makimbilio Healing Centre’.
Mwenyekiti wa Kamati ya Amani Mkoa wa Shinyanga Sheikh Balilusa Khamis akizungumza katika Kanisa la EAG (T) Ushirika Shinyanga ‘Makimbilio Healing Centre’.
Askofu Mkuu wa Kanisa la EAG (T) Dkt. Brown Abel Mwakipesile (kushoto) akiteta jambo na Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Dkt. Philemon Sengati baada ya kuweka Wakfu Jengo la Kanisa la EAG (T) Ushirika Shinyanga ‘Makimbilio Healing Centre’ leo Jumapili Oktoba 3,2021.
Picha zote na Kadama Malunde – Malunde 1 blog