Katibu Mkuu Wizara ya Afya Prof. Abel Makubi,akizungumza na watumishi wa Wizara ya Madini wakati akiwapatia elimu kuhusiana na chanjo dhidi ya UVIKO-19 ili kuwajengea uelewa kuhusu chanjo hiyo kikao kilichofanyika jijini Dodoma.
Baadhi ya washiriki wakifatilia mada kutoka kwa Katibu Mkuu Wizara ya Afya Prof. Abel Makubi,wakati akitoa elimu kwa watumishi wa Wizara ya Madini kuhusiana na chanjo dhidi ya UVIKO-19 ili kuwajengea uelewa kuhusu chanjo hiyo kikao kilichofanyika jijini Dodoma.
……………………………………………………………………..
Na.Alex Sonna,Dodoma.
Katibu Mkuu Wizara ya Afya Prof. Abel Makubi ameanza kuelimisha watumishi wa umma kwenye idara na taasisi za umma kuhusu chanjo dhidi ya UVIKO-19 ili kuwajengea uelewa kuhusu chanjo hiyo.
Hayo ameyasema jijini Dodoma wakati wa kikao cha kawaida cha Watumishi wa Wizara ya Madini ,Prof.Makubi amesema jamii inapaswa kuelimishwa kuhusina na chanjo.
Prof. Makubi amesema lengo la kuanza kutoa elimu kwa watumishi wa umma na binafsi ni kutokana na nafasi zao ya kutofikiwa na wataalam wa afya ambao wameanza kutoa elimu hiyo ngazi ya jamii.
“Jamii inapaswa kuelimishwa kuhusiana na chanjo huku akitoa wito kwa wafanayakzi wa Wizara ya Madini kuchanja lakini pia kwa wafanyakazi wote wa serikali na kuachana na fikila potofu zinazosambazwa na watu wasiopenda maendeleo ya nchi.
“kwa kuwadhibitishia toka tumezindua mpango wa jamii shirikishi vijijini na mijini Septemba 15,2021 watu wameelimika na wanachanja kwa wingi kwa siku watu wanakuwa Zaidi ya elfu 30000 kabla ya elimu hii kwa siku walikuwa wanakuwa elfu 20000 na kupungua,”amesema Prof.Makubi
Prof.Makubi amesema kuwa Serikali ina malengo mazuri kwa wananchi wake ndio maana wanaendelea kwalinda kwa kuwapa elimu kuhusiana na Chanjo na haiwezi kuwaacha wananchi katika janga hili.
Aidha Prof.Makubi ametoa wito kwa wananchi kuendelea kupata chanjo ili kuweza kujilinda pamoja na kuendelea kujikinga na ugonjwa wa Covid -19 na kuchukua tahadhari zote zinazotolewa na Wizara ya afya.
Kwa upande wake Mmoja ya washiriki wa elimu hiyo mfanyakazi wa wizara ya madini,Tibishena Wamburaa , amesema amepata elimu kuhusiana na chanjo hiyo hivyo anawatoa hofu waliokuwa na wasiwasi kuhusu kupata chanjo ya Covid.
“Nimepata elimu niliokuwa nahitaji Prof.Makubi ametuelimisha vyema na amenitoa hofu hivyo nitakuwa balozi mzuri pamoja na kuwa mshauri ili niweze kutoa elimu kwa watu waliokuwa wanahofu kuhusiana na chanjo ya Covid 19”amesema Wambura