WAZIRI wa Nchi,Ofisi ya Rais,Utumishi na Utawala Bora Mohammed Mchengerwa,akizungumza wakati akifungua kikao kazi cha Watendaji Wakuu wa Wakala za Serikali (hawapo pichani) kilichofanyika leo September 30,2021 jijini Dodoma.
WAZIRI wa Nchi,Ofisi ya Rais,Utumishi na Utawala Bora Mohammed Mchengerwa,akisisitiza jambo kwa washiriki wakati wa kikao kazi cha Watendaji Wakuu wa Wakala za Serikali (hawapo pichani) kilichofanyika leo September 30,2021 jijini Dodoma.
Katibu Mkuu, Wizara ya Katiba na Sheria Prof. Sifuni Mchome kwa niaba ya Katibu Mkuu-UTUMISHI ,akizungumza wakati wa kikao kazi cha Watendaji Wakuu wa Wakala za Serikali kilichofanyika leo September 30,2021 jijini Dodoma.
Baadhi ya Watendaji Wakuu wa Wakala za Serikali wakimsikiliza Waziri wa Nchi,Ofisi ya Rais,Utumishi na Utawala Bora Mohammed Mchengerwa,(hayupo pichani) wakati akifungua kikao kazi cha Watendaji Wakuu wa Wakala za Serikali kilichofanyika leo September 30,2021 jijini Dodoma.
Mkurugenzi wa Idara ya Uchambuzi na Ushauri wa Kazi, Ofisi ya Rais-UTUMISHI, Bw. Nolasco Kipanda akitoa neno la utangulizi kabla ya Waziri wa Nchi,Ofisi ya Rais,Utumishi na Utawala Bora Mohammed Mchengerwa,kufungua kikao kazi cha Watendaji Wakuu wa Wakala za Serikali kilichofanyika leo September 30,2021 jijini Dodoma.
Mtendaji Mkuu na Mkuu wa Chuo cha Utumishi wa Umma, Dkt. Emmanuel Shindika akitoa neno la shukrani kwa niaba ya washiriki kwa Waziri wa Nchi,Ofisi ya Rais,Utumishi na Utawala Bora Mohammed Mchengerwa,mara baada ya kufungua kikao kazi cha Watendaji Wakuu wa Wakala za Serikali kilichofanyika leo September 30,2021 jijini Dodoma.
Waziri wa Nchi,Ofisi ya Rais,Utumishi na Utawala Bora Mohammed Mchengerwa,akiwa katika picha ya pamoja na washiriki mara baada ya kufungua kikao kazi cha Watendaji Wakuu wa Wakala za Serikali kilichofanyika leo September 30,2021 jijini Dodoma.
………………………………………………………………
Na.Alex Sonna,Dodoma
WAZIRI wa Nchi,Ofisi ya Rais,Utumishi na Utawala Bora Mohammed Mchengerwa amewaagiza watendaji wa ofisi yake kuwashusha vyeo Maafisa Utumishi katika Taasisi za Umma walioshindwa kuwapandisha vyeo watumishi wenye sifa za kupanda madaraja.
Kauli hiyo ameitoa leo September 30,2021 jijini Dodoma wakati akifungua kikao kazi cha Watendaji Wakuu wa Wakala za Serikali chenye lengo la kuhimiza uwajibikaji kwa watendaji hao.
Amesema,kuwa Afisa Utumishi yeyote aliyezembea na kusababisha Watumishi wa Umma kutopandishwa madaraja achukuliwe hatua kwa kushushwa cheo na kuhamishwa kituo cha kazi ili iwe ni fundisho kwa wengine wanaoshindwa kuwajibika ipasavyo.
“Fanyeni upembuzi na kuwaondoa Maafisa Utumishi wote waliobainika kutotekeleza wajibu wa kuwapandisha madaraja watumishi wenye sifa stahiki, kwani nimekuwa nikipokea malalamiko toka kwa watumishi wa taasisi mbalimbali,” amesema Mhe. Mchengerwa
Aidha amefafanua kuwa, ofisi yake ilifanya kazi usiku na mchana kuhakikisha taarifa za kiutumishi zilizotumwa na waajiri zinafanyiwa kazi kwa lengo la kuwapandisha vyeo watumishi husika.
“Mhe. Rais anatambua kuwa nguzo ya Serikali kiutendaji ni Watumishi wa Umma hivyo haiwezi kufanya vizuri iwapo haitowajali watumishi wake na ndio maana aliagiza wapandishwe madaraja,” Mhe. Mchengerwa amefafanua.
Aidha Waziri Mchengerwa amewataka watendaji hao kutotumia mwanya wa kuajiri vibarua au watumishi wa mkataba kama njia ya kuweka mwanya wa watumishi hewa.
“Ndugu zangu niwaambie katika bajeti ya 2021/2022 serikali iliomba kibali cha kuajiri watumishi 46,000 na mpaka sasa waliojiriwa hawazidi 10,000, hivyo kama watendaji mnauhitaji wa wafanyakazi ombeni kibali cha kuajiri na sio kutumia vibarua au watumishi wa mkataba ili kuweka mwanya wa watumishi hewa,”amesisitiza
Kwa upande wake Katibu Mkuu wa Wizara ya Katiba na Sheria Profesa Sifuni Mchome amesema kuwa lengo la kikao hicho ni kujadili masuala ya wakala ,mafanikio pamoja na changamoto na hatimaye kuzitafutia ufumbuzi wa namna ya kuzitatua.
“Uwepo wa wakala umeleta mafanikio mengi,mojawapo ni wakala nyingi zimeboresha huduma ambapo zinatolewa kwa muda mfupi na bora,wakala nyingi zimeongeza wigo wa mapato ya ndani na kuweza kujitegemea,”amesema
Naye Mtendaji Mkuu na Mkuu wa Chuo cha Utumishi wa Umma, Dkt. Emmanuel Shindika,akitoa neno la shukrani kwa niaba ya washiriki amemshukuru Mhe. Waziri kwa kukubali wito wa kukutana na Watendaji Wakuu wa Wakala za Serikali na kumuahidi kutekeleza maelekezo yote aliyoyatoa.