Home Biashara INFINIX NA TIGO WASHIRIKIANA KUZINDUA Infinix ZERO X PRO TANZANIA

INFINIX NA TIGO WASHIRIKIANA KUZINDUA Infinix ZERO X PRO TANZANIA

0

Mkuu wa Kitengo cha Maduka na Bidhaa za Intaneti Tigo Tanzania Bw. Mkumbo Myonga (kulia), Afisa Uhusiano wa Infinix, Aisha Karupa wakiwa katika picha ya pamoja.

Afisa Uhusiano wa Infinix, Aisha Karupa akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam kuhusu uzinduzi wa Infinix ZERO X PRO TANZANIA.

Mkuu wa Kitengo cha Maduka na Bidhaa za Intaneti Tigo Tanzania Bw. Mkumbo Myonga (kushoto), Afisa Uhusiano wa Infinix, Aisha Karupa wakizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam kuhusu uzinduzi wa Infinix ZERO X PRO TANZANIA.

*******************

NA NOEL RUKANUGA, DAR ES SALAAM.

Kampuni inayoongoza kwa utoaji wa Huduma za Kidigitali hapa nchini Tigo Tanzania imeshirikiana na Infinix Tanzania kuzindua simu janja toleo jipya yenye kiwango cha juu ya 108MP na 60x kamera, ijulikanayo kama Infinix ZERO X PRO, ambayo itauzwa kuanzia 800,000 Tsh.

Akizungumza jijini Dar es Salaam wakati wa kutangaza simu hiyo Mkuu wa Kitengo cha maduka na Bidhaa za Intaneti Tigo Tanzania Bwana Mkumbo Myonga amesema kuwa “Ushirikiano wa Tigo na Infinix Tanzania unaonyesha zaidi lengo la kuunganisha nguvu na kuwa Vinara katika utoaji wa huduma za Kidigitali nchini Tanzania, kwa kuongeza upatikanaji wa simu bora sokoni zitakazochochea kuongezeka kwa huduma za Kidigitali.

Myonga pia ameongeza kuwa, “kuzindua Infinix Zero X PRO kunadhiirisha kwamba wateja wa Tigo watajipatia kilicho bora, suala litakalochangia kuongeza thamani ya mazingira ya kibiashara nchini.”

Kulingana na Myonga “Simu hizo zinapatikana katika maduka yote ya Tigo nchini kote na zitakua na Ofa ya GB 96 za Intaneti Bure kutumia mwaka mzima. “

Afisa Uhusiano wa Infinix, Aisha Karupa, alisema kuwa “kutangazwa kwa toleo jipya la simu ya Infinix zero x pro kunadhiirisha maana halisi ya teknolojia maana teknolojia inahusisha Uvumbuzi wa bidhaa mpya na kuvuka mipaka zaidi na zaidi ili kuwafikia wateja kiurahisi na Infinix ZERO X pro inamwezesha mtumiaji kufanya vitu vingi kwa pamoja maana ina processor ya Helio G95 kwa ajili ya kucheza GAME ,”

Bi Aisha pia ameongeza “Infinix zero x pro imethibitishwa na Royal Observatory Greenwich ya jijini londoni kuwa MP 108 IOS na zoom lens ya 60X periscope ya Infinix ZERO X pro imefaulu katika jaribio la kupija picha ya mwezi ANGANI.

Infinix ZERO X pro sasa inapatikana katika maduka ya Infinix na Tigo nchi nzima.