WAZIRI wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Dk.Ashatu Kijaji,akizungumza wakati akifungua semina ya kujenga uelewa na kuhamasisha utekelezaji wa mfumo wa anwani za makazi kwa Jumuiya ya Serikali za Mitaa kwa Mameya,Wenyeviti na Wakurugenzi wa Majiji na Halmashauri za Wilaya iliyofanyika leo September 29,2021 jijini Dodoma.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Dk.Zainab Chaula,akizungumza wakati wa semina ya kujenga uelewa na kuhamasisha utekelezaji wa mfumo wa anwani za makazi kwa Jumuiya ya Serikali za Mitaa kwa Mameya,Wenyeviti na Wakurugenzi wa Majiji na Halmashauri za Wilaya iliyofanyika leo September 29,2021 jijini Dodoma.
Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, TAMISEMI, Prof.Riziki Shemdoe,akizungumza wakati wa semina ya kujenga uelewa na kuhamasisha utekelezaji wa mfumo wa anwani za makazi kwa Jumuiya ya Serikali za Mitaa kwa Mameya,Wenyeviti na Wakurugenzi wa Majiji na Halmashauri za Wilaya iliyofanyika leo September 29,2021 jijini Dodoma.
WAZIRI wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Dk.Ashatu Kijaji,akiteta jambo na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Dk.Zainab Chaula,wakati wa semina ya kujenga uelewa na kuhamasisha utekelezaji wa mfumo wa anwani za makazi kwa Jumuiya ya Serikali za Mitaa kwa Mameya,Wenyeviti na Wakurugenzi wa Majiji na Halmashauri za Wilaya iliyofanyika leo September 29,2021 jijini Dodoma.
WAZIRI wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Dk.Ashatu Kijaji,akiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kufungua semina ya kujenga uelewa na kuhamasisha utekelezaji wa mfumo wa anwani za makazi kwa Jumuiya ya Serikali za Mitaa kwa Mameya,Wenyeviti na Wakurugenzi wa Majiji na Halmashauri za Wilaya iliyofanyika leo September 29,2021 jijini Dodoma.
………………………………………………………..
Na.Alex Sonna,Dodoma
Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Dk.Ashatu Kijaji amewataka Mameya,Wenyeviti na Wakurugenzi kuwashirikisha madiwani,watendaji wa kata vijiji na mitaa ili kuhakikisha kila eneo nchini linakuwa na anwani ya makazi.
Amesema Wizara yake imejipanga hadi kufikia mwaka 2025 huduma za anwani ya makazi ziwe zimefika katika kila eneo nchini.
Kauli hiyo ameitoa leo September 29 Jijini Dodoma wakati akifungua semina ya kujenga uelewa na kuhamasisha utekelezaji wa mfumo wa anwani za makazi (Postikodi) kwa Mameya,Wenyeviti na Wakurugenzi wa Majiji na Halmashauri za Wilaya.
Waziri Kijaji amesema Mameya,Wenyeviti na Wakurugenzi wanatakiwa kuwashirikisha madiwani,watendaji wa kata vijiji na mitaa ili kuhakikisha kila eneo nchini linakuwa na anwani ya makazi.
“Twendeni tukawashirikishe madiwani kila mmoja akashirikishe jamii yake, watendaji wa kata, vijiji, mitaa ili kufikia haya, Tanzania imeamua kuingia kwenye dunia ya kidigitali,”amesema Dk.Kijaji.
Amesema kuwa licha ya changamoto inazokutana nazo imejipanga mpaka ifikapo mwaka 2025 huduma za anwani ya makazi ziwe zimefika katika kila eneo nchini.
Hata hivyo amesema hadi kufikia mwezi huu asilimia tatu ya kata zote zilizopo nchini zilikuwa zimefikiwa na huduma hiyo hivyo amezitaka Halmashauri kushiriki ipasavyo kwenye jukumu hilo ili kata zote zifikiwe na huduma hiyo.
Dk.Kijaji amesema kuwa asilimia hiyo tatu ni ya kata 135 kati ya 4,067 zilizopo nchini ambapo kwa Zanzibar zipo 110.
Dk.Kijaji amemshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuweza kutoa fedha kwa ajili ya zoezi hilo.
Hata hivyo Waziri Kijaji amesema kuwa Wizara ya Habari imepewa sh.bilioni 45 kwa ajili ya uratibu wa kuweka anwani hizo huku Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) ikipewa zaidi ya Sh.Bilioni 100 na hivyo kuwataka viongozi hao kusafiri kwa pamoja kukamilisha kazi hiyo.
“Sisi kama waratibu tunasema tutasafiri na yule atakayekuwa na kasi kwenye utekelezaji, twende kwa pamoja, tusafiri kwa pamoja, Wizara ya Ardhi wapo tayari kwenye kupima,”amesema
Dk.Kijaji amesema kuwa mfumo huo unarahisisha wananchi kushiriki moja kwa moja kwenye shughuli za maendeleo ya kijamii.
“Dunia yetu kwasasa inaelekea kwenye uchumi wa kidigitali, kuna kufanya biashara kwa njia ya mtandao, unafanya mawasiliano kwa njia ya mtandao na unaletewa bidhaa yako hadi nyumbani,”amesema.
Hata hivyo amesema kuwa hatua hiyo itasaidia kukuza uchumi kwa kuwa watanzania hawatapoteza muda wao kufuatilia bidhaa au huduma.
Kwa upande wake Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Dk.Zainab Chaula, amesema wamejipanga ifikapo mwaka 2025 kuhakikisha kila nyumba inakuwa namba yake.
Amesema kila Mamlaka za Serikali za Mitaa na Mkurugenzi ana bajeti lakini utekelezaji wake ni wa kusuasua,ambapo ameipongeza Halmashauri ya Jiji la Mwanza kwa kufanya kazi kubwa mpaka sasa.
Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, TAMISEMI, Prof.Riziki Shemdoe, alisema zimeandaliwa sheria ndogo zitakazotumiwa na Halmashauri kusimamia utekelezaji wa mfumo huo wa anwani za makazi.
Prof.Shemdoe amesema kuwa postikodi zote zimeandaliwa na kuingizwa kwenye kanzidata,Halmashauri 21 zimeshajengewa uwezo juu ya maudhui ya mfumo huo.
“Imeandaliwa program tumizi kwa ajili ya kuhakikisha utoaji huduma za kiuchumi na kijamii pamoja na kusimamia utoaji wa huduma, rasimu ya utekelezaji wa mfumo huu umeandaliwa,”amesema .
Aidha amesema kuwa shughuli za uingizaji wa anwani ya makazi zimeingizwa kwenye mwongozo wa bajeti na kuhimiza Halmashauri kutenga fedha kwa ajili hiyo.