Home Michezo YANGA YAANZA VYEMA LIGI KUU,YAICHAPA 1-0 KAGERA SUGAR MJINI BUKOBA

YANGA YAANZA VYEMA LIGI KUU,YAICHAPA 1-0 KAGERA SUGAR MJINI BUKOBA

0

Mabingwa wa Kihistoria wa Ligi Kuu Tanzania bara timu ya Yanga imeanza vyema Ligi  Kuu ya Tanzania Bara baada ya kuichapa  bao 1-0 Kagera Sugar katika  Uwanja wa Kaitaba,Mjini Bukoba Mkoani Kagera.

Shujaa wa Yanga alikuwa Kiungo Mshambuliaji  Feisal Salum Abdallah ‘Fei Toto’ dakika ya 24 akifunga   bao hilo kwa shuti la mguu wa kushoto akimalizia mpira uliookolewa na kipa Issa Chalamanda kufuatia shuti la awali la mshambuliaji Mkongo, Fiston Mayele Kalala.
Mechi nyingine ya Ligi Kuu leo, mabao ya mshambuliaji Vitalis Mayanga dakika ya tatu na 20 yameipa Polisi Tanzania ushindi wa 2-0 dhidi ya KMC Uwanja wa Black Rhino, Karatu mkoani Arusha.