Meneja wa shule ya mchepuo wa kiingireza ya Hady nursery ,primary na secondari,Ruth Muniko akizungumza mara baada ya mahafali shuleni hapo Jana.(Happy Lazaro)
***********************************
Happy Lazaro,Arusha
Arusha.Wazazi kwa kushirikiana na jamii kwa ujumla wametakiwa kwa pamoja kusimamia na kuendeleza maadili ya watoto wao pindi wanaporudi majumbani huku wakitumia muda mwingi kuzungumza nao katika kujiepusha na makundi yasiyofaa.
Hayo yamesemwa na Meneja wa shule ya mchepuo wa kiingireza ya Hady nursery,primary na secondary ,Ruth Muniko wakati akizungumza na wanafunzi pamoja na wazazi katika mahafali ya darasa la saba ambapo jumla ya wanafunzi 70 walihitimu masomo yao.
Muniko amesema kuwa, wazazi wana wajibu mkubwa katika kufuatilia maadili ya watoto wao kwa karibu hususani katika kipindi hiki ambacho wapo majumbani kwani wanahitaji uangalizi wa karibu Sana ili wasipotoshwe na makundi mabaya.
“Tunawaomba Sana wazazi hivi Sasa watoto hawa wameshatoka mikononi mwetu ,naomba mkawasimamie kwa karibu kwani huko mtaani kuna vishawishi vingi tunajua mpo bize katika kutafuta maisha lakini tengeni muda wa kuzungumza nao sambamba na kuwafuatilia pia ili waweze kufikia ndoto zao za baadaye na kuyaendeleza maadili yote waliyofundishwa hapa shuleni.”amesema.
Aidha amewataka wazazi kuhakikisha wanatenga muda wa kuzungumza nao na kujua changamoto zinazowakabili kwani kwa Sasa hivi wapo mikononi mwao huku wakihakikisha wanawaeleza ukweli kuhusu hali ya maisha ilivyo hususani wanapokuwa mtaani na kuepukana na vishawishi mbalimbali.
Hata hivyo Muniko amewataka wahitimu hao kutambua kuwa huo sio mwisho wa elimu ndo kwanza wameanza wahakikishe wanaongeza juhudi na bidii katika masomo yao ili kila mmoja aweze kufikia malengo yake aliyojiwekea.
“Nawaomba Sana watoto wangu leo mmehitimu darasa la Saba mjue ndo mmeanza safari ongezeni bidii Kama ambavyo mlikuwa mkifanya hapa katika kuhakikisha kila mmoja wenu anafikia malengo yake huku mkijiepusha na makundi yasiyofaa sambamba na vishawishi mbalimbali popote mtakapokuwa.”amesema Muniko.
Naye Mzazi mwakilishi ambaye pia ni Mjumbe wa kamati ya shule,Lugalata Kalamu amesema kuwa,watoto hao wamesoma katika shule hiyo kwa miaka saba na wameonyesha nidhamu na maadili ya hali ya juu,hivyo akiwataka wazazi kuhakikisha wanayaendeleza yale yote yaliyokuwa yakifanywa na watoto hao wakiwa shuleni.
Kalamu amewataka wazazi na walezi kwa pamoja kuwa mstari wa mbele kuendeleza ndoto za watoto hao badala ya kuwakatisha tamaa kwani kwa kufanya hivyo kutawawezesha kila mmoja kufikia ndoto zake na kuondokana na vishawishi mbalimbali.