Home Mchanganyiko DKT. NDUMBARO AWATAKA WATUMISHI WA UMMA KUUTUMIKIA UMMA KWA UZALENDO, UADILIFU NA...

DKT. NDUMBARO AWATAKA WATUMISHI WA UMMA KUUTUMIKIA UMMA KWA UZALENDO, UADILIFU NA WELEDI

0

Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Dkt. Laurean Ndumbaro akifungua kikao kazi cha ofisi yake na Taasisi zinazosimamia Maadili na vyama vya kitaaluma chenye lengo la kubadilishana uzoefu wa usimamizi wa maadili, kilichofanyika Ukumbi wa Ofisi ya Rais-UTUMISHI Mtumba jijini Dodoma.

Baadhi ya washiriki wa kikao kazi cha Taasisi zinazosimamia Maadili na vyama vya kitaaluma chenye lengo la kubadilishana uzoefu wa usimamizi wa maadili wakimsikiliza Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais-UTUMISHI Dkt. Laurean Ndumbaro (hayupo pichani) wakati akifungua kikao kazi hicho kilichofanyika Ukumbi wa Ofisi ya Rais-UTUMISHI Mtumba jijini Dodoma.

Mkurugenzi wa Idara ya Ukuzaji Maadili, Ofisi ya Rais-UTUMISHI, Bi. Leila Mavika (wa kwanza kushoto) akitoa neno la utangulizi wakati wa ufunguzi wa kikao kazi cha ofisi yake na Taasisi zinazosimamia Maadili na vyama vya kitaaluma chenye lengo la kubadilishana uzoefu wa usimamizi wa maadili, kilichofanyika Ukumbi wa Ofisi ya Rais-UTUMISHI Mtumba jijini Dodoma.

Baadhi ya washiriki wa kikao kazi cha Taasisi zinazosimamia Maadili na vyama vya kitaaluma chenye lengo la kubadilishana uzoefu wa usimamizi wa maadili, wakifuatilia moja ya mada iliyowasilishwa na Mkurugenzi wa Idara ya Ukuzaji Maadili, Ofisi ya Rais-UTUMISHI, Bi. Leila Mavika  katika kikao kazi hicho kilichofanyika Ukumbi wa Ofisi ya Rais-UTUMISHI Mtumba jijini Dodoma.

Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Dkt. Laurean Ndumbaro akiwa katika picha ya pamoja na washiriki wa kikao kazi cha Taasisi zinazosimamia Maadili na vyama vya kitaaluma chenye lengo la kubadilishana uzoefu wa usimamizi wa maadili mara baada ya kukufungua kikao kazi hicho, kilichofanyika Ukumbi wa Ofisi ya Rais-UTUMISHI Mtumba jijini Dodoma.

*********************************

Na Veronica Mwafisi-DODOMA

Tarehe 29, Septemba, 2021

 

Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Dkt. Laurean Ndumbaro amewataka Watumishi wa Umma nchini kuutumikia umma kwa uzalendo, uadilifu na weledi ili kutimiza azma ya Serikali ya kutoa huduma bora kwa wananchi.

Dkt. Ndumbaro ametoa wito huo wakati akifungua kikao kazi cha siku mbili cha taasisi simamizi za maadili na vyama vya kitaaluma chenye lengo la kubadilishana uzoefu wa usimamizi wa maadili, kilichofanyika katika ukumbi wa Ofisi ya RaiS-UTUMISHI Mtumba, jijini Dodoma.

Dkt. Ndumbaro amesema uzalendo, uadilifu na utendaji kazi unaozingatia weledi ndio nguzo kuu ya utendaji kazi wa Watumishi wa Umma ikiwa ni pamoja na ustawi wa taifa.

Ameongeza kuwa, ofisi yake imekuwa na utamaduni endelevu wa kushirikiana na taasisi zinazosimamia maadili na vyama vya kitaaluma ili kujenga taifa imara lenye Watumishi wa Umma wazalendo na waadilifu.

“Ushirikiano uliopo kati ya ofisi yangu na taasisi simamizi za maadili na vyama vya kitaaluma, utasaidia kujenga uadilifu kwenye utumishi wa umma na jamii kwa ujumla”, Dkt. Ndumbaro amefafanua.

Dkt. Ndumbaro amesema, Watumishi wa Umma nchini wanao wajibu wa kuunga mkono kwa vitendo azma ya Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan ya kuujenga Utumishi wa Umma kuwa wenye kuzingatia uadilifu, uwajibikaji, Kanuni, Sheria, Taratibu na miongozo iliyopo.

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Idara ya Ukuzaji Maadili, Ofisi ya Rais-UTUMISHI, Bi. Leila Mavika amesema lengo kuu la kikao kazi hicho ni kukumbushana uzingatiaji wa maadili, kujadili changamoto za usimamizi wa maadili katika Utumishi wa Umma na kuzitafutia ufumbuzi.

Mwanasheria wa Bodi ya Wataalamu ya Ununuzi na Ugavi, Bw. Suleiman Mzava ambaye ni mmoja wa washiriki wa kikao kazi hicho amesema, kikao kazi hicho kitasaidia kujenga uadilifu miongoni mwa taasisi za umma hivyo ameipongeza Serikali kwa kuweka nguvu kubwa katika usimamizi wa maadili.

Watumishiwa Umma wa wakizingatia uzalendo, uadilifu na weledi katika utekelezaji wa majukumu yao ya kila siku, watatoa huduma bora kwa wananchi na kutoa mchango mkubwa katika maendeleo ya taifa.