………………………………………………………………
Na: Grace Kisyombe,ARUSHA
Shirika la umeme Tanzania (TANESCO) limekuwa mwenyeji wa mkutano wa watendaji wa mashirika kumi na moja yanayo zalisha kusafirisha na kusambaza umeme katika nchi za Afrika mashariki na kati. Mkutano ambao unafanyika katika Hoteli ya Palace iliyopo katika jiji la Arusha .
Katika mkutano huo, Wawakilishi wa kutoka Nchi kumi na moja katika ukanda wa Afrika Mashariki na Kati wamekutana nchini Tanzania kujadili namna ya kukabiliana, kutatua changamoto ya upatikanaji wa nishati ya umeme wa uhakika wenye gharama nafuu kwa wananchi wa nchi wanachama wa ( East African power pool ) . Mkutano ulio na lengo la kuziunganisha nchi wanachama kupitia makampuni yanayo zalisha , kusafirisha na kusambaza umeme Afrika Mashariki .
Akizungumza katika mkutano huo, Mwakilishi wa Shirika la umeme Tanzania (TANESCO )Mhandisi Philipo Lalisa ambaye ni Kaimu Meneja mwendeshaji wa mifumo ya umeme katika gridi ya Taifa amesema Muunganiko wa nchi hizo unasaidia namna ya matumizi mazuri ya vyanzo vya umeme katika nchi wanachama ambapo Tanzania ni miongoni mwa nchi yenye vyanzo vya aina mbalimbali za uzalishaji umeme. Mhandisi Lalisa pia amesema Serikali ya Tanzania kupitia TANESCO inaendelea na maandalizi kuwezesha kuongeza upatikanaji umeme katika ukanda wa Afrika Mashariki, ambapo TANESCO inaendelea na ujenzi wa njia kuu ya usafirishaji umeme wa msongo wa kilovolti 400 utakao iunganisha nchi yetu na nchi ya Kenya kwa upande wa kaskazini ambapo ndipo umoja huu wa afrika mashariki unafikiwa pia kwa upande wa kusini mradi huu utaiwezesha TANESCO kusafirisha umeme hadi nchini Zambia kupitia tunduma , jambo ambalo linaiwezesha nchi yetu kujiunga pia katika umoja wa makampuni yanayo uziana umeme kusini mwa Afrika (south African power pool) hivyo kuwezesha nchi yetu kuuza umeme katika nchi za afrika mashariki pamoja na zile zilizo kusini mwa Afrika .
Naye Katibu Mkuu wa Kamati tendaji ya nchi washirika kupitia muungano wa makampuni yanayozalisha,kusafirisha na kusambaza umeme katika nchi za afrika mashariki na kati (Eapp) Bw.Lebbi Kisitu amesema kwa sasa mkutano huu umelenga kujadili nama ya kufanya biashara baina ya nchi hizo kwa kuwa katika makubaliano ya pamoja endapo nchi moja itanunua umeme kutoka nchi zilizopo katika muungano huo.
Bwana Kisitu amesema kwa sasa ujenzi wa miundombinu ya kusafirisha na kusambaza nishati hiyo katika nchi wanachama unaendelea ambapo kwa sasa wanaendelea na makubaliano ya pamoja kama washirika na baadae mwezi Octoba mwaka huu 2021, wajumbe wa kamanti tendaji ya East African power pool wanatarajia kukutana na Mawaziri wa Nishati kutoka katika nchi za Tanzania , Kenya ,Uganda,Sudani, Ethiopia , Djibout, DRC –Congo, Burundi , pamoja na nchi za Misri na Libya , watakao pokea taarifa ya majadiliano yanayo endelea sasa.
Mwakilishi mwingine kutoka nchi ya Rwanda Bw. Wilson Karegyeya amesema pamoja na ushirika huu nchi washirika zitapata fursa ya kuuziana umeme kwa gharama na fuu sambamba na kutumia miundombinu ya nchi husika katika kusafirisha umeme kutoka nchi moja hadi nyingine endapo itatokea uhitaji wa kufanya hivyo
Miongoni mwa faida ambazo Tanzania itapata kupitia ushirika huu ni pamoja na kuuza umeme kwa nchi wanachama pindi Mradi mkubwa wa kuzalisha umeme wa megawati 2115 wa Julius Nyerere utakapo kamilika mapema Juni mwaka 2022. Mradi ambao ni wa pili kwa ukubwa kwa nchi wanachama wa East African power pool , Hali itakayo liongezea shirika la TANESCO mapato sambamba na kuwezesha wananchi wa Tanzania kuwa na umeme wa kutosha wakati wote hivyo kukuza uwekezaji katika shughuli za viwanda, sekta ya uchimbaji madini pamoja na Kilimo.