Nibu waziri wa Mambo ya Ndani ambae pia ni Mbunge wa Jimbo la Uzini Khamis Hamza Chilo akizungumza na viongozi wa Chama cha Mapinduzi na Jumuiya zake (hawapo pichani) katika kikao cha kutathimini shughuli za Kimaendeleo huko ukumbi wa Mikutano Machui.
Mwakilishi wa Jimbo la Uzini Haji Shaaban Wazir akimkabidhi zawadi ya Kanga kutoka kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Samia Suluhu Hassan mmoja wa madiwani wa Viti maalum kutoka Jimbo la Uzini..
Mbunge wa Jimbo la Uzini Khamis Chilo na Mwakilishi Haji Shaaban kwa pamoja wakikunjua kanga ilionapicha ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Samia Suluhu Hassan ikiwa ni Zawadi kutoka kwa Rais huyo kwa Viongozi wa Jimbo la Uzini huko ukumbi wa mikutano Machui.
Viongozi mbali mbali wa Chama na Jumuiya za Chama cha Mapinduzi wakisikiliza kwa Makini Viongozi wa Jimbo la Uzini (hawapo pichani) wakati wa kikao cha kutathimini shughuli za Kimaendeleo huko ukumbi wa Mikutano Machui.
PICHA NA BAHATI HABIBU MAELEZO ZANZIBAR
………………………………………………………………….
BAHATI HABIBU MAELEZO ZANZIBAR
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani Khamis Hamza Chilo ambae ni Mbunge wa Jimbo la Uzini amewataka wananchi wa Zanzibar kuunga mkono juhudi za Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapimduzi Dkt. Husein Ali Mwinyi za kuwaweka Wazanzibari kuwa wamoja ili kufikia maendeleo ya Uchumi wa Buluu.
Ametoa kauli hiyo huko Machui Jimbo la Uzini wakati akizungumza na Viongozi wa Chama Cha Mapinduzi na Jumuiya zake katika kikao cha kutathmini shughuli za kimaendeleo zilizofanywa na Viongozi wa Jimbo hilo.
Amesema ili kufikia maendeleo ya Uchumi wa Buluu Zanzibar ni vyema wazanzibari kuungana pamoja bila ya kujali tofauti zao za kisiasa, dini na kuulinda umoja na mshikamano uliokuwepo tokea kufanyika kwa Mapindunzi ya Zanzibar na Muungano wa Tanganyika na Zanzibar.
Aidha amewahimiza viongozi hao kuwa waadilifu na kupanga mipango madhubuti itakayosaidia kukipa ushindi Chama Cha Mapinduzi katika chaguzi zake za ndani zinazotarajiwa kufanyika mwaka 2022 na kuchagua Viongozi waliyobora kwa uchaguzi wa mwaka 2025 kutoka ndani ya Chama hicho.
Akizungumzia maendeleo yaliyoletwa na viongozi wa Jimbo hilo ni pamoja na kusambaza umeme katika Kijiji cha Kiboje na Bambi Kijibwe Mtu, kusambaza mipira ya maji, kuchimba Visima, kujenga minara na kueka matenki ya kuhifadhia maji kwa vijiji viliyokuwa vinakosa huduma hiyo muhimu .
Nae Mwakilishi wa Jimbo hilo Haji Shaaban Waziri amesema viongozi wa Jimbo hilo wamekusudia kuondosha changamoto ya uhaba wa vyumba vya madarasa kwa kujenga madarasa mapya na kufanya ukarabati kwa baadhi ya Skuli zinazovuja ili kusaidia wanafunzi kupata Elimu iliyobora .
Akitaja Skuli ambazo zimejengwa na zipo hatua ya mwisho kukamilika ni pamoja na Skuli ya Msingi Mchangani, Ujenzi wa vyumba sita vya madarasa, Skuli ya Bambi Msingi, Vyumba vinane vya kusomea na Skuli ya Msingi Koani, vyumba sita vya madarasa na ukumbi wa kufanyia Mitihani katika Skuli ya Msingi Kidimni.
Aidha ameeleza kuwa Viongozi wa Jimbo hilo kwa kusaidiana na wafadhili mbali mbali wa maendeleo wanatarajia kujenga kiwanja cha Michezo katika Kijiji cha Bambi kitakachokuwa na uwezo wa kukusanya watu 10000 kwa wakati mmoja sambamba na nyumba watakazofikia wanamichezo.