Home Mchanganyiko MBIO ZA MWENGE WA UHURU ZAPITISHA MIRADI YOTE YA TANGANYIKA

MBIO ZA MWENGE WA UHURU ZAPITISHA MIRADI YOTE YA TANGANYIKA

0

Wanafunzi wa shule ya Msingi Ifukutwa waliounda klabu ya kupinga dawa za kulevya wakitoa ujumbe wakati Mbio maalum za Mwenge zilipofika shuleni hapo

Kiongozi wa kitaifa wa mbio maalum za mwenge wa uhuru 2021 Luteni Josephine Mwambashi wa pili kulia akiangalia kiwanda cha pamba Ifukutwa, kulia kwake ni mkuu wa wilaya ya Tanganyika Onesmo Busweru

………………………………………………………….

Na. Zillipa Joseph Katavi

Mbio maalum za Mwenge wa Uhuru umekagua na kupitisha miradi yote ya wilaya ya Tanganyika iliyoandaliwa kupitia na mwenge huo mwaka huu 2021 zikiwemo klabu za dawa za kulevya

Aidha miradi mingine iliyopitiwa na Mwenge huo maalum ni pamoja na Mradi wa maji wa Ifukutwa, kiwanda cha pamba na barabara

Akitoa salamu kwa wananchi mara baada  ya kukagua mradi wa maji wa Ifukutwa Kiongozi wa Mbio Maalum za Mwenge 2021 Luteni Josephine Mwambashi amewataka wananchi kuutunza mradi huo

Lt. Mwambashi amesema serikali imetumia fedha nyingi kwa ajili ya kuwapatia huduma ya maji safi hivyo ni wajibu wao kuutunza na endapo kutatokea tatizo lolote basi watoe taarifa kwa wasimamizi ili lishughulikiwe

Mradi huo unahudumia zaidi ya wakazi 10,627 wa vijiji vya Ifukutwa, Igalula Na Mchakamchaka

Akitoa taarifa kwa kiongozi wa Mbio Maalum za Mwenge Kitaifa Meneja wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira (RUWASA) wilaya ya Tanganyika Mhandisi Alkam Sabuni amesema mradi huo umegharimu kiasi cha shilingi bilioni 1.57

Mhandisi sabuni ameongeza kuwa licha ya watu kuchota maji katika vituo maalu vilivyojengwa pia wanasambaza maji katika nyumba zinzotaka huduma hiyo majumbani na mpaka sasa wamekwishasambaza kwa nyumba 44

Aidha katika kiwanda cha kuchakata pamba kilichopo Ifukutwa Kiongozi huyo wa mbio za Mwenge alimpongeza mwekezaji na kusema kuwa kuwepo kwa kiwanda hicho kumewezesha wakulima wa pamba mkoani katavi kuwa na soko la uhakika

Pia amewataka wakulima kuongeza bidii katika kilimo cha pamba