Kikosi cha wachezaji 24 , Benchi la ufundi Pamoja na viongozi 10 wa klabu ya KMC FC , kitaondoka jijini Dar es salaam kesho asubuhi kuelekea mkoani Kilimanjaro kwa ajili ya mchezo wa kwanza wa Ligi kuu soka Tanzania bara msimu wa 2021/2022 dhidi ya Polisi Tanzania utakaochezwa Septemba 29 katika uwanja wa Ushirika Moshi mkoani humo.
Kwa mujibu wa ratiba ya Bodi ya Ligi kuu Tanzania (TPLB) mara baada ya pazia kufunguliwa , KMC FC itakuwa ugenini kwa michezo miwili ambapo ni dhidi ya Polisi Tanzania utakaopigwa Septemba 29 na mwingine ni dhidi ya Coastal Union ya Mkoani Tanga utakaochezwa Oktoba mbili katika Dimba la Mkwakwani.
Kikosi hicho cha Manispaa ya Kinondoni, Chini ya kocha Mkuu ,Mkongwe John Simkoko na wasaidizi wake Habibu Kondo, Hamadi Ally kimefanya maandalizi ya kutosha katika kipindi chote cha majuma manne tangu kuanza kwa maandalizi ya msimu mpya (Pre season) ambapo awali iliweka kambi mkoani Morogoro na kumalizia Jijini Dar es salaam.
Katika kipindi cha maandalizi (Pre season), klabu hiyo ya wana Kino Boys imefanya maandalizi kwa ufasini mkubwa na kwamba matarajio ni kuhakikisha kuwa Timu inapata matokeo mazuri katika michezo miwili ya ugenini kwakuanza na ule wa Septemba 29 dhidi ya Polisi Tanzania ambao utapigwa 14:00 mchana.
“Tangu tulipoanza maandalizi kwa wachezaji wetu, kikosi kimefanya mazoezi ya kutosha na hasa ukizingatia kwamba tunakwenda kuanza ligi ambayo kimsingi inaushindani mkubwa, lakini kwa ujumla tumejiandaa kukabiliana na ushindani huo na matarajio yetu ni kuhakikisha tunakwenda kufanya vizuri katika michezo yetu.
Kipindi cha maandalizi (Pre season) tumekitumia kwa mafanikio makubwa ambayo kimsingi tunaweza kusema kwamba tumekaa na wachezaji wote na hivyo kujenga ule muunganiko wapamoja ukizingatia tunamaingizo mapya ya wachezaji hivyo kikubwa tunakwenda sasa kupambana kwa jitihada zetu,wachezaji pamoja na benchi zima la ufundi ili kupata matokeo mazuri katika michezo yote tuliyokuwanayo msimu huu.