Home Michezo ZAO JIPYA LA UTALII WA MCHEZO WA GOFU LILILOZINDULIWA KUONGEZA IDADI YA...

ZAO JIPYA LA UTALII WA MCHEZO WA GOFU LILILOZINDULIWA KUONGEZA IDADI YA WATALII NCHINI

0
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt.Damas Ndumbaro akiwa amepiga mpira wa gofu huku akifuatilia muelekeo wa mpira huo huku washiriki wakishuhudia mara baada ya mgeni rasmi  Waziri wa Utalii na Wanyamapori wa Kenya, Mhe.Najib Balala kuzindua utalii huo wa gofu ambalo ni zao jipya la utalii nchini, uzinduzi huo mefanyika jana katika viwanja vya Kiligofu Jijini Arusha

Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt.Damas Ndumbaro ( kulia)  akizungumza na Wachezaji waenzake mchezo wa  gofu mara baada ya mgeni rasmi  Waziri wa Utalii na Wanyamapori wa Kenya, Mhe.Najib Balala   kuzindua utalii huo wa gofu ambalo ni zao jipya la utalii nchini, uzinduzi huo mefanyika jana katika viwanja vya Kiligofu Jijini Arusha, Wa kwanza kushoto ni Kamishna Uhifadhi wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania, Prof.Dos Santos Silayo

Waziri wa Utalii na Wanyamapori wa Kenya, Mhe.Najib Balama akizungumza na baadhi ya Washiriki wa mchezo wa gofu wa kutoka ndani na nje ya nchi  mara baada ya kuzindua utalii huo ambao ni zao jipya la utalii nchini  uliofanyika jana katika viwanja vya Kiligofu Jijini Arusha.Wa pili kushoto ni Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt.Damas Ndumbaro.


Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt.Damas Ndumbaro ( wa pili kushoto)  akiwa kwenye picha  pamoja na Wachezaji waenzake wa mchezo wa  gofu mara baada ya mgeni rasmi  Waziri wa Utalii na Wanyamapori wa Kenya, Mhe.Najib Balala   kuzindua utalii huo wa gofu ambalo ni zao jipya la utalii nchini, uzinduzi huo umefanyika jana katika viwanja vya Kiligofu Jijini Arusha.


Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt.Damas Ndumbaro ( kulia)  akimuonesha  mgeni rasmi  Waziri wa Utalii na Wanyamapori wa Kenya, Mhe.Najib Balala  baadhi ya hoteli zilizopo katika uwanja wa Gofu wa Kiligofu  mara baada ya kuzindua utalii huo wa gofu ambalo ni zao jipya la utalii nchini, uzinduzi huo mefanyika jana katika viwanja vya Kiligofu Jijini Arusha.

Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt.Damas Ndumbaro akizungumza na Wachezaji wenzake  mchezo wa  gofu mara baada ya mgeni rasmi  Waziri wa Utalii na Wanyamapori wa Kenya, Mhe.Najib Balala   kuzindua utalii huo wa gofu ambalo ni zao jipya la utalii nchini, uzinduzi huo mefanyika jana katika viwanja vya Kiligofu Jijini Arusha,  Wengine ni Viongozi kutoka Wizara ya Maliasili na Utalii pamoja na Taasisi zilizo chini ya wizara hiyo.

Waziri wa Utalii na Wanyamapori wa Kenya, Mhe.Najib Balala akizindua utalii wa gofu ambalo ni zao jipya la utalii nchini huku akiwa anashuhudiwa na Washiriki mbalimbali wa mchezo huo kutoka ndani na nje ya nchi katika uzinduzi huo uliofanyika jana katika viwanja vya Kiligofu Jijini Arusha.Wa tatu kulia ni Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt.Damas Ndumbaro.
………………………………………………………………
Na Mwandishi Maalumu, Arusha.
 
ZAO jipya la Utalii wa mchezo wa gofu uliozinduliwa mapema 25 Septemba mwaka huu Jijini Arusha, kuongeza idadi ya Watalii nchini kama ilani ya Chama cha Mapinduzi (CCM ) ilivyoelekeza, Wizara ya Maliasili na Utalii.
 
Hayo yamebainishwa Jijini hapa na, Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Damas Ndumbaro ambapo pia amesema juhudi kubwa za kimkakati zilizoendeshwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe.Samia Suluhu Hassan kupitia Royal Tour, zimeweza kuchagiza ubunifu wa kimkakati katika Wizara hiyo ili kwenda sambamba na maono ya Mhe.Rais ya  kuongezeka idadi ya watalii nchini.
 
”Mimi kama Waziri pamoja na Watendaji wote katika Wizara ninayoiongoza shabaha yetu kubwa ni kuona idadi ya watalii inaongezeka kwa kuibua na kubuni mazao ya utalii ambayo ni mapya hapa kwetu” alisisitiza Dkt. Ndumbaro
 
Aidha, Dkt. Ndumbaro amemshukuru  kwa mara nyingine Mhe Rais kwa kuonesha njia katika sekta hiyo  na wao kupitia wizara ya Maliasili na Utalii kilichobaki ni utekelezaji ikiwemo  kuanzia pale Mhe.Rais alipoishia.
 
Kwa upande wake, Waziri wa Utalii na Wanyamapori wa Kenya, Mhe.Najib Balala ambaye alikuwa ni mgeni rasmi katika uzinduzi huo wa Utalii kupitia mchezo wa gofu wa siku mbili 25-26 Septemba, unaofanyika  katika viwanja vya Kiligolf Jijini hapa, amesema mchezo huo  unaowakutanisha watu kutoka mataifa mbalimbali duniani ambao huja kwa ajili ya kucheza na kuongezeka pato litokanalo na utalii.
 
“Kwetu sisi nchini Kenya mchezo wa gofu umekuwa na mwamko mkubwa na tumekuwa na mashindano makubwa yanayowakutanisha washiriki kutoka  mataifa mbalimbali duniani kila mwaka” alisisitiza Waziri Mhe. Najibu Balala.
 
Ameongeza kuwa, uzinduzi  huo wa mchezo wa gofu utachochea watalii kukaa kwa muda mrefu nchini kwa vile watalii watakuja kwa ajili ya kuona   wanyamapori lakini pia wataongeza siku ya zaidi ya siku  mbili kwa ajili ya kucheza mchezo huo.
 
Amesema mpango wa nchi ya Kenya ni kutaka kuona Tanzania inafanikiwa kufungamanisha michezo na utalii ili ziweze kushirikiana ambapo wachezaji wa gofu watakaocheza Kenya waje pia kucheza mchezo huo nchini Tanzania.
 
Waziri Mhe Balala amesema mkakati huo endapo utaweza kufanikiwa utasaidia kuongeza idadi ya watalii na kupunguza utegemezi wa kufikiria kuwa utalii pekee ni ule wa kuona wanyamapori pekee yake.
 
Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Bodi yaTaifa ya Utalii ( TTB) Jaji ( Mst) Thomas Mihayo amesema uzinduzi wa utalii wa gofu umekuja wakati muafaka ambapo Mhe.Rais amekuwa akionesha njia na kuita Wawekezaji kutoka nchi za nje kuja kuwekeza nchini.
 
“Leo hii Mataifa 13 yameshiriki na tunaamini Washiriki hawa watakaporudi nchini kwao watakuwa mabalozi wazuri mbali ya kueleza walivyoshiriki katika mchezo huo bali wataelezea uzuri wa Tanzania” alisema Jaji Mihayo.
 
Kwa upande wake, Martin Kiula ambaye ni mshiriki wa mchezo huo amewatoa wasi wasi watu wanaoshindwa kujifunza mchezo huo wakifikiria kuwa mchezo huo ni maalum kwa ajili ya watu matajiri pekee.
 
Katika uzinduzi huo jumla ya Wachezaji ambao ni watalii 140 kutoka nchi 13 duniani wameshiriki na wanatarajia kukaa nchini kwa zaidi ya siku tano ikiwa ni mkakati wa kuongeza idadi ya Watalii kutoka milioni 1.5  hadi kufikia watalii milioni 5 ifikapo mwaka 2025
 
Uzinduzi huo wa Utalii kupitia mchezo wa Gofu unatarajiwa kufikia tamati leo 26 Septemba kwenye viwanja hivyo vya Kiligolf, Jijini hapa Arusha.