Mkuu wa Wilaya ya Iringa Mohamed Hassan Moyo akiliagiza Jeshi la polisi pamoja na TAKUKURU kufanya uchunguzi dhidi ya Mwenyekiti wa Kijiji Cha Welu anayedaiwa kujihusisha na vitendo Vya rushwa na kumaliza Kesi za ubakaji Kiholela.
Na
Fredy Mgunda,Iringa.
Mkuu
wa Wilaya ya Iringa Mohamed Hassan Moyo ameagiza Jeshi la polisi pamoja na
TAKUKURU kufanya uchunguzi dhidi ya Mwenyekiti wa Kijiji Cha Welu anayedaiwa
kujihusisha na vitendo Vya rushwa na kumaliza Kesi za ubakaji Kiholela.
Akiwa
kwenye mkutano wa hadhara mkuu wa wilaya hiyo,waliibuka baadhi ya Wananchi
wakimtaja mwenyekiti Ponsian Makapa amekuwa akishughulikia kesi za ubakaji na
nyinginezo na kuzimaliza kwa kupokea rushwa jambo ambalo ni kinyume na
sheria za nchi.
Moyo
alisema kuwa malalamiko ya wananchi kuonewa na kiongozi huyo hayapaswi
kufumbiwa macho na hasa tukio na mwanamke mmoja kubakwa na wanaume wa wawili
ambalo Kesi yake pia ilimalizwa Kiholela.
Alisema
kuwa miongoni mwa Kesi zinazotajwa kumalizwaa kiholela ni pamoja na kesi ubakaji
inayowahusisha vijana wawili Mathayo Ngeng`ena na Bidan Mkuvasa wanaodaiwa
kushirikiana kumbaka mwanamke mmoja mkazi wa Kijiji hicho Cha Welu kata Ulanda
Mkoani Iringa.
Moyo
alisema haiwezekani kesi ya ubakaji inamalizika kirahisi hivyo huku ushaidi
ukiwepo kwa wanaume hao wawili kumbaka mama moja mwenye watoto watatu anaishi
katika kijiji hicho na kesi hiyo ikaisha kirahisi na watuhumiwa kuachiwa huru
na kuendelea na kazi zao kama kawaida.
Alisema
kuwa utamaduni uliojengeka kwa wahalifu kuendeleza vitendo hivyo wakijivunia
Kutofikishwa kwenye vyombo vya Dola ama kutochukuliwa hatua stahiki za kisheria
haukubariki hata kidogo
Kesi
za kijamii ikiwemo zinazohusisha migogoro ya wanakijiji na zinatajwa kuwa
sehemu ya Mwenyekiti huyu Ponsian Makapa kujipatia fedha isivyo halali na
kuendelea kuzusha manung’uniko kwa Wananchi wa kijiji cha Welu.
Awali
wakitoa malalamiko kwa mkuu wa wilaya ya Iringa baadhi ya wananchi walisema
kuwa kiongozi huyo amekuwa anakikiuka sheria,taratibu,na kanuni za kuongoza
kijiji hicho kwa kuendekeza rushwa ambazo zimekuwa zinawaumiza baadhi ya
wananchi wa kijiji hicho.
Walisema
kuwa kumekuwa na kesi za ubakaji,mimba za utotoni,unyanyasaji wa kijinsia na
uongozi usio bora unaopelekea kuvunjika kwa amani katika kijiji hicho ambacho
wananchi wake wamekuwa wanakihusisha na kilimo kwa asilimia kubwa.
Wananchi
hao walisema kuwa kushamili kwa vitendo hivyo kumesababisha wananchi wengi hasa
wanawake na mabinti kuogopa kwenda kuokota kuni porini wakihofia kubakwa kama
ambavyo wengine wamekuwa wakifanyiwa na wanaume wa kijiji hicho.
Kwa
upande wa Mwenyekiti wa Kijiji Cha Welu Ponsian Makapa alikanusha tuhuma hizo
na kusema kuwa sio kweli anazushiwa tu kutokana na tatizo la maswala ya kisiasa
hasa walewanaoitaka nafasi yake.
Hata
hivyo Mkuu wa Wilaya ya Iringa Mohamed Moyo akatoa maagizo ya kufanyika
uchunguzi dhidi ya madai yote yanayomkabili Kiongozi huyo wa Kijiji
Kando
ya hayo amesisitiza uwajibikaji bora kwa viongozi wa Serikali serikali za
mitaa,vijiji,kata na tarafa na kuwataka kuacha mara moja kufanya kazi kwa
mazoea la sivyo atawapeleka polisi wao.
Tatizo
la ubakaji na mimba za utotoni limeendelea kuwa janga kwa wananchi wa wilaya ya
Iringa kutokana na baadhi ya wanaume kuendelea kufanya vitendo hivyo huku vitendo
hivyo vimekuwa havichukulikiwi kwa uzito unaostahili na viongozi wa vijiji,kata na tarafa kwa ujumla
wakati sheria za vitendo hivyo zipo wazi.
Nao jeshi la polisi wilaya ya
Iringa walisema kuwa wameyapokea maagizo ya mkuu wa wilaya na watayafanyia kazi
kama ambavyo yanatakiwa kufanyiwa kazi kwa mjibu wa sheria