Home Michezo TP MAZEMBE YAITIA DOA SHEREHE YA SIMBA DAY, YAICHAPA BAO 1-0 SIMBA...

TP MAZEMBE YAITIA DOA SHEREHE YA SIMBA DAY, YAICHAPA BAO 1-0 SIMBA SC KWENYE UWANJA WA MKAPA

0

**************************

NA EMMANUEL MBATILO,DAR ES SALAAM.

Klabu ya Simba leo ilikuwa inahitimisha wiki ya  Simba Day ambapo sherehe wameifanyika katika uwanja wa Benjamini Mkapa Jijini Dar es Salaam ambapo wau maarufu wameudhiuria hafla hiyo akiwemo spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Job Ndugai.

Katika hafla hiyo pia kulikuwa na tukio la kutambulisha wachezaji wao ambao wataitumikia klabuu hiyo msimu huu unaoanza mwezi ujao.

Mchezo wa kirafiki ulichezwa ambapo Simba Sc iliwaalika TP Mazembe kutoka nchini Kongo ambapo Simba imepokea kichapo cha bao 1-0.