Home Michezo RASMI YANGA YAONDOLEWA LIGI YA MABINGWA AFRIKA, YACHAPWA 1-0 NA RIVERS UNITED

RASMI YANGA YAONDOLEWA LIGI YA MABINGWA AFRIKA, YACHAPWA 1-0 NA RIVERS UNITED

0
 
 
*********************************
 
Klabu ya Yanga rasmi yaaga mashindano ya Kimataifa kwenye michuano ya CAF Championi League ambapo baada ya kupokea kichapo cha jumla ya mabao 2-0 dhidi ya Rivers United mara baada ya mechi ya kwanza kufungwa bao 1-0 kwenye uwanja wa Benjamini mkapa jijini Dar es Salaam.
 
Yanga ilikwenda nchini Nigeria kwa matumaini ya kupindua matokeo baada ya meci ya kwanza kufungwa bao 1-0 lakini wameshindwa kufurukuta baada ya kutembezewa tena kichapo cha bao 1-0 kwenye mchezo ambao ulikuwa na sintofahamu nyingi.
 
Yanga watarudi usiku huu Jijini Dar es Salaam kujiandaa na mchezo unaofuata dhidi ya watani wao Simba Sc kwenye ngao ya hisani ambapo mchezo utapigwa mwishoni mwa mwezi huu.