Baadhi ya Wajasiriamali wanaowezeshwa na Barrick wakionesha bidhaa zao katika moja ya maonyesho ya biashara
Baadhi ya Wajasiriamali wanaowezeshwa na Barrick wakionesha bidhaa zao katika moja ya maonyesho ya biashara
Baadhi ya Wajasiriamali wanaowezeshwa na Barrick wakionesha bidhaa zao katika moja ya maonyesho ya biashara
Baadhi ya Wajasiriamali wanaowezeshwa na Barrick wakionesha bidhaa zao katika moja ya maonyesho ya biashara
**
Kuna msemo maarufu wa Kichina usemao kuwa Usimpe mtu samaki, mfundishe kuvua ili asiendelee kuomba Samaki bali avue mwenyewe.Kampuni ya madini ya Barrick inatekeleza msemo huu kwa vitendo kutokana na kutekeleza programu ya kuwapatia wajasiriamali wanaoishi karibu na migodi yake ijulikanayo kama ‘Biashara yangu biashara yako’.
Mafunzo haya ambayo hutolewa na wataalamu wa masuala ya biashara na ujasiriamali yamefanikiwa kuwawezesha wajasiriamali wengi wa maeneo hayo hususani wanawake kusimama kiuchumi na kuendesha shughuli zao kwa utaalamu na kujiamini.
Wajasiriamali ambao wamenufaika na programu ya mafunzo haya, ni wale wanaojishughulisha na kilimo, ufugaji wa kuku, wazalishaji wa uyoga,ushonaji,watengeneza nguo za batiki, mafundi ujenzi na shughuli nyingineo nyingi.
Katika mahojiano yaliyofanyika karibuni, mmoja wa wanufaika wa progarmu hii,Clementina Felix, mkazi wa Bugarama wilayani Kahama, anayejishughulisha na biashara ya ushonaji kwa niaba ya wenzake ,aliishukuru kampuni ya Barrick, kwa uwezeshaji mkubwa inaofanya kwa wajasiriamali wa wilaya hiyo kwa kuwapatia mafunzo ya biashara na kuwaunga mkono katika shughuli zao za ujasiriamali.
“Barrick, inawezesha wajasiriamali zaidi ya 200 kutoka vijiji 14 vilivyopo katika kata za Mwingiru, Bulyanhulu na Bugarama, ambapo tumekuwa tukipatiwa mafunzo ya biashara na kuwezeshwa kushiriki maonyesho mbalimbali pia bidhaa tunazozalisha soko letu kubwa tunalitegemea kutoka kwa wafanyakazi wa mgodini”, alisema Clementina.
Akiwa fundi wa ushonaji anasema amefanikiwa kubuni makoti ambayo yanavutia watu wengi katika soko, ambapo pia amefankiwa kupata soko kutoka kampuni ya Barrick kwa ajili ya wafanyakazi wake na amekuwa na masoko ya nje ambayo amekuwa akiyapata kutokana na kuwezeshwa kushiriki katika maonyesho mbalimbali ya biashara.
Aliongeza kuwa katika kipindi hiki cha mlipuko wa ugonjwa wa UVIKO 19,wapo wajasiriamali wenzake ambao wanashona barakoa na kuweza kuziuaza katika masoko mbalimbali na kujikwamua kiuchumi sambamba na kuboresha maisha ya familia zao ikiwemo kuboresha makazi yao na kusomesha watoto.
Mjasiriamali mwingine,Berita Nyawanga anasema kuwa tangu aanze kuhudhuria mafunzo yanayotolewa na Barrick kupitia programu ya Biashara yangu biashara yako ,shughuli zake zinaenda vizuri na ameweza kugundua kuwa sio mtai pekee unahitajika kufanikiwa kibiashara bali mafunzo ya uendeshaji biashara ni muhimu na ndio nguzo kubwa ya mafanikio.
Nyawanga, aliongeza kusema kuwa Barrick imeleta ukombozi katika maeneo yao, hususani kwa wanawake ambao walibaki nyuma katika shughuli za kujikwamua kiuchumi lakini kwa sasa wamekuwa na mwamko mkubwa kushiriki katika shughuli za ujasiriamali na wanaweza kujipatia vipato badala ya kuwa tegemezi kwa wenzawao kama ilivyokuwa hapo awali.
Kwa upande wake Ester Lali, ambaye anashughulika na ufugaji wa nyuki katika kijiji cha Kakola wilayani Kahama,alisema Barrick, inaendelea kuwezesha wana vijiji kuchangamkia ufugaji wa nyuki kupitia kuwaleta wataalamu wa kuwafundisha ufugaji bora wa nyuki.
“Mwamko wa ufugaji wa nyuki unaendelea kuwa mkubwa na wapo wafugaji wameanza kupata asali bora na wanaendelea kuiuza katika masoko mbalimbali nchini na kinachofurahisha anawake wengi na vijana wanaendelea kujitokeza kuchangamkia fursa hii”,alisema Lari.
Afisa Mahusiano ya Jamii wa Barrick Bulyanhulu, Sebastian Antony, amesema programu ya mafunzo ya biashara kwa wajasiriamali imepokelewa vizuri na inaendelea kuwanufaisha,ambapo wapo ambao biashara zao zinazidi kukua siku hadi siku na baadhi yao wamefikia hatua ya kuzalisha ajira kutokana na shughuli zao.
Antony alisema kuwa pia wanavijiji wanaoishi jirani na mgodi kupitia mafunzo haya wameweza kutambua fursa za kibiashara zilizopo katika maeneo yao ambapo wameanza kuzichangamkia na kuweza kujipatia vipato kupitia kujiajiri.
Barrick imedhamiria kuhakikisha wananchi wanaoishi jirani na maeneo yake ya kazi wanaendelea kunufaika na shughuli za uchimbaji wa madini, kupitia sera ya ushirikishwaji wananchi katika mnyororo wa madini kupitia kupewa kipaumbele katika kuuza na kutoa huduma migodini.