Naibu Katibu Mkuu wa CCM (Bara) Ndugu Christina Mndeme akiangalia nguvu ya maji wakati alipotembelea mradi wa maji Makonde uliopo Newala mkoani Mtwara.
………………………………………………..
Naibu Katibu Mkuu wa CCM (Bara) Ndugu Christina Mndeme amemtaka Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji kufika Newala siku ya jumatatu tarehe 20 Septemba, 2021 katika mradi wa maji Makonde ambao haujatoa maji kwa takribani wiki tatu sasa.
Akizungumza mara baada ya kutembelea kituo cha kupokea maji kutoka kwenye chanzo cha maji Mkunya na kujionea mashine zikiwa zimeharibika.
Naibu Katibu Mkuu alisema”Tukiri kuna uzembe umefanika hapa katikati haiwezekani mashine tangu mwaka 1954 mpaka leo zinatumika”
Ndugu Mndeme amesema maji hayana mbadala na amesikitishwa sana kuona hakuna hatua zinazochukuliwa kwa haraka katika kutatua tatizo la maji wilayani hapo.
Naibu Katibu Mkuu ameshangazwa na kuona fedha kiasi cha bilioni 11 zimepelekwa na Serikali lakini mradi haujafanyiwa marekebisho mpaka sasa.
Naibu Katibu yupo kwenye ziara ya Katibu Mkuu wa CCM pamoja na Wajumbe wa Sekretarieti ya Halmashauri Kuu ya CCM yenye lengo la kukagua, kusimamia na kuhamasisha utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya CCM ya mwaka 2020-2021.