Mkurugenzi wa Taasisi ya Raising Up Friendndiship Foundation (RUFFO) Bi.Hilda Ngaja akizungumzia semina maalumu ya Elimu ya Fedha kwa watoto wenye umri chini ya miaka 18 iliyofanyika jijini Dar es Salaam.
Meneja wa Program wa Taasisi ya Raising Up Friendndiship Foundation (RUFFO) Bi. Magdalena Thomas akichangia mada katika semina maalumu ya Elimu ya Fedha iliyotolewa kwa watoto wenye umri chini ya miaka 18.
Afisa Masoko wa UTT AMIS, Bi. Ester Kahabi akitoa mafunzo kwa watoto namna ya kufanya Uwekezaji. UTT AMIS ni Taasisi ya Serikali iliyo chini ya Wizara ya Fedha na Mipango na dhumuni kuu ya kuanzishwa kwake ni kuendeleza Mifuko ya Uwekezaji wa pamoja hapa nchini.
Mkaguzi wa Hesabu kutoka KMC Associate Bi. Paulina George akitoa mafunzo kwa watoto namna ya kupanga bajeti na kubana matumizi ya Fedha katika semina maalumu iliyoandaliwa na Taasisi ya Raising Up Friendndiship Foundation (RUFFO) jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya watoto wenye umri chini ya miaka 18 wakishiriki semina maalumu ya matumizi ya Fedha iliyoandaliwa na Taasisi ya Raising Up Friendship Foundation (RUFFO) Jijini Dar es Salaam
*****************************
NA NOEL RUKANUGA, DAR ES SALAAM.
Wazazi na walezi wametakiwa kuwa na utamaduni wa kuwafundisha watoto elimu ya fedha jambo ambalo litawasaidia katika maisha kufanikiwa kiuchumi kuwa wawekezaji katika nyanja mbalimbali.
Akizungumza leo jijini Dar es Salaam katika semina maalamu ya kuwajengea uwezo wototo katika kupanga bajeti, kubana matumizi ya fedha na kufanya uwekezaji, Mkurugenzi wa Taasisi ya Raising Up Friendndiship Foundation (RUFFO) Bi.Hilda Ngaja, amesema kuwa ni vizuri jamii ikawa na utaratibu wa kuwapa elimu watoto ambayo itawasaidia katika maisha yao.
Bi. Ngaja amesema kuwa semina hiyo imewasaidia watoto walioshiriki ambayo imelenga kuwahamasisha kuwa na tabia nzuri ya matumizi ya fedha, kupanga bajeti ambayo rafiki kwa watu wenye lengo la kufanya uwekezaji.
“Watoto hawafanyi kazi ya kuingiza kipato lakini wanapewa fedha na wazazi wao kwa ajili kufanya matumizi madogo madogo, kupitia fedha hizo tunawafundisha tabia ya kuweka akiba na kubana matumizi ili ziwasaidia baadaye” amesema Bi. Ngaja.
Amefafanua kuwa wapo baadhi ya watu wamekuwa na tabia kufanya matumizi makubwa ya fedha kuliko kipato chao, jambo ambalo sio rafiki kwani wengi wamekuwa wakirudi nyuma kimaendeleo.
“Baadhi ya wanafunzi wa chuo wakipewa fedha za matumizi baada ya muda mfupi fedha zote amezitumia, hii inatokana na kukosa elimu ya fedha tangu akiwa mtoto” amesema Bi. Ngaja.
Mkurugenzi huyo ameishauri Serikali na wadau mbalimbali kuwe na utaratibu wa kutoa elimu ya fedha kuanzia shule za awali ili kuwajenga tabia watoto ya kuwa matumizi mazuri ya fedha ili waje kuwa wawekezaji na kupanua fursa za ajira.
Mkaguzi wa Hesabu kutoka KMC Associate Bi. Paulina George, amesema kuwa wametoa elimu ya kupanga bajeti kutokana watoto ni msingi, hivyo wakifundishwa tangu wadogo jinsi ya kuwa na nidhamu ya fedha, kutafuta fedha itawasaidia kuwa na uwelewa mpana.
“Watoto wakiwa na elimu ya fedha itawasaidia kuheshimu fedha pamoja na wazazi wanaotafuta fedha…baadhi tayari wamekuwa na mawazo ya kupanga bajeti” amesema Bi. George.
Bi. Geoge katika semina hiyo alikuwa mkufudhi wa somo la bajeti, kupana matumizi ya fedha, ambapo amewataka wazazi wawe na utamaduni wa kuwashirikisha watoto namna ya kupanga bajeti kabla ya kufanya matumizi.
Afisa Masoko wa UTT AMIS Bi. Ester Kahabi, amesema kupata elimu ya uwekezaji ukiwa mdogo ni vizuri kwani wakiwa wakubwa wanaweza kulifanyika kazi kwa vitendo.
“Baadaye watoto watakuwa wawekezaji, kwani bado tuna mipango ya kuendelea kutoa elimu ili kuwafikia watoto watu wengi” amesema Bi. Kahabi.
Hata hivyo amewataka wazazi kuju UTT AMIS kwani ni taasisi ya Serikali iliyo chini ya Wizara ya Fedha na Mipango na dhumuni kuu ya kuanzishwa kwake ni kuendeleza Mifuko ya Uwekezaji wa pamoja hapa nchini.
Ameeleza kuwa kuna Mfuko wenye dhumuni la kuwanufaisha watoto kwa ajili ya maisha yao ya baadaye kutokana elimu ni gharama hivyo ni vyema kuanza kuwawekea akiba mapema.
Taasisi ya Raising Up Friendndiship Foundation (RUFFO) imekuwa ikitoa elimu ya kuwajenga uwezo wa watoto katika nyanja mbalimbali kwa lengo la kuwaelimisha kwa ajili ya maisha yao.