Home Siasa MZEE WA KILWA AGUSWA NA ZIARA MASHINANI

MZEE WA KILWA AGUSWA NA ZIARA MASHINANI

0

Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Ndg. Daniel Chongolo akiendelea na ziara yake Mkoani Lindi, amekutana na Mzee Mohamed Angema ambaye ameguswa na utaratibu huo wa Chama kutembelea, Kukagua Uhai wa Chama na kusikiliza Wanachama ngazi za Mashina (Mabalozi).

Akizungumza mbele ya Katibu Mkuu kwa ufupi alipopewa fursa ya kutoa maoni, ushauri, changamoto na kuomba dua katika mkutano wa shina namba 4 Kata ya Kiranjeranje Wilayani Kilwa, Mzee Angema amesifu utaratibu huo wa Chama kwa kusema;

“Nchi hii tuimarishe Chama, Chama kinapambwa na nchi inapambwa, Chama kama hakikupamba nchi yake hatutafanikiwa, kupambwa kwa nchi, wananchi wenyewe washibe, msione hasara kuhangaika na shida za watu, thawabu kubwa tuipate kwa Mungu, utaratibu huu unaoufanya (Katibu Mkuu) wa kutembelea Mashina hatujawahi kuuona na naomba muendelee hivo”.

Huu ni Muendelezo wa Ziara inayofanywa na Katibu Mkuu akiambatana na Wajumbe wa Sekretarieti ya Halmshauri Kuu ya CCM Taifa, Mkoani Lindi na Kuendelea katika Mikoa ya Mtwara, Ruvuma na Njombe.