Barbara Gonzalez Afisa Mtendaji wa Klabu ya Simba SC ya jijini Dar es Salaam pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Ndege la ATCL Injini Ladslaus Matindi wakionesha mkataba mara baada ya kuasini kufuatia Klabu hiyo na shirika la ndege nchini (ATCL) kuingia makubaliano ya ushirikiano wa kibiashara utakaowawezesha Simba SC kusafiri ndani na nje ya Tanzania kwa ndege za shirika hilo pekee.
Mbali na hilo mkataba huo wenye thamani ya shilingi milioni 400 pia unatajwa kuwanufaisha mashabiki wa timu hiyo kwa kuwekea mfumo maalum wa kupata usafiri wa ndege kwa wepesi kwa ajili ya kwenda kuiunga mkono timu ya Simba SC inapocheza nchini Tanzania na nje ya nchi.
Hafla hiyo imefanyika kwenye makao makuu ya ATCL mtaa wa Ohio jijini Dar es Salaam.
Barbara Gonzalez Afisa Mtendaji wa Klabu ya Simba SC ya jijini Dar es Salaam pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Ndege la ATCL Injini Ladslaus Matindi wakitia saini mkataba huo utakaozinufaisha pande zote mbili.
Barbara Gonzalez Afisa Mtendaji wa Klabu ya Simba SC ya jijini Dar es Salaam pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Ndege la ATCL Injini Ladslaus Matindi wakibadilishana mkataba mara baada ya kuasini kufuatia Klabu hiyo na shirika la ndege nchini (ATCL) kuingia makubaliano ya ushirikiano wa kibiashara utakaowawezesha Simba SC kusafiri ndani na nje ya Tanzania kwa ndege za shirika hilo pekee.
Barbara Gonzalez Afisa Mtendaji wa Klabu ya Simba SC ya jijini Dar es Salaam akizungumza katika hafla hiyo iliyofanyika kwenye makao makuu ya ATCL jijini Dar es Salaam kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Ndege la ATCL Injini Ladslaus Matindi
Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Ndege la ATCL Injini Ladslaus Matindi akifafanua jambo mara baada ya kusainiwa kwa mkataba huo kushoto ni Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano ATCL Bw. Josephat Kagirwa
Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Klabu ya Simba Bw. Ezekiel Kamwaga akihojiwa na Mtangazaji wa AZAM TV Timzo Karugira kabla ya kuanza kwa hafla hiyo.