NA MWANDISHI WETU, GEITA
Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF) umesema utayatumia Maonesho ya Nne ya Teknolojia na Uwekezaji katika Sekta ya Madini yanayofanyika Mkoani
Geita kutoa elimu na kuwahudumia wanachama wake na wananchi kwa ujumla.
Maonesho hayo yaliyobeba kauli mbiu isemayo “ Sekta ya Madini kwa Ukuaji wa Uchumi na
Maendeleo ya Watu,” yameanza Septemba
16, 2021 kwenye eneo la EPZ lililoko Bombambili Mkoani humo na yatafikia kilelele
Septemba 26.
Akizungumzia ushiriki wa Mfuko kwenye Maonesho hayo, Meneja wa PSSSF Mkoa wa Geita, Bw. Geofrey
Kolongo, alisema Maonesho hayo ambayo huandaliwa na Mkoa na kufanyika kila
mwaka ni fursa nzuri kwa Mfuko kukutana na wanachama wake na wananchi kwa
ujumla ili kutoa huduma na elimu kuhusu masuala ya Hifadhi ya Jamii.
Alisema
Wanachama wa PSSSF ni watumishi wote wa Umma na watumishi wote wa Mashirika na
Taasisi ambazo Serikali ina Hisa zaidi ya Asilimia 30.
“Kwa
muktadha huo, utaona wanachama wetu wengi wako hapa na tumejipanga kutoa elimu
kuhusu Mafao mbalimbali yatolewayo na Mfuko ikiwemo Pensheni za kila mwezi,
Fao la uzazi, Fao la kukosa Ajira, Taarifa kuhusu Michango ya mwanachama, Mstaafu
anaweza kuhakiki taarifa zake, Taarifa kuhusu uwekezaji lakini pia kuna huduma nyingine ya kidigitali, PSSSF Kinganjani na PSSSF ulipo mtandaoni .” Alifafanua
Bw.Kolongo.
Akieleza
zaidi alisema, Mwanacham au mwananchi mwingine yoyote akifika kwenye banda letu
atahudumiwa kama ambavyo anavyohudumiwa kwenye ofisi zetu za PSSSF zilizosambaa
nchi nzima Bara na Visiwani.
Mfuko
wa PSSSF ulianza Tarehe 1 Agosti, 2018 baada ya Serikali kuunganisha Mifumo
Minne ya PPF,PSPF, LAPF na GEPF.
Meneja wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF)
Mkoa wa Geita, Bw. Geofrey Kolongo
(kulia), akimhudumia mwanachama alietembelea banda ya PSSSF katika maonesho ya
Teknilojia ya Madini eneo la Bomba Mbili viwanja vya EPZA Mkoani hum oleo Septemba
17, 2021.
Meneja wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma
(PSSSF) Mkoa wa Geita, Bw. Geofrey
Kolongo (kulia), akizungumzia huduma mbalimbali zitolewazo na PSSSF kwenye
maonesho hayo.