Home Mchanganyiko DKT.TAX AFUNGA MAFUNZO YA SIKU TANO YA WAJUMBE WA KAMATI YA KUDUMU...

DKT.TAX AFUNGA MAFUNZO YA SIKU TANO YA WAJUMBE WA KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA MAMBO YA NJE,ULINZI NA USALAMA

0

Waziri wa Ulinzi na jeshi la kujenga taifa Dkt. Stargomena Tax akizungumza wakati akifunga mafunzo ya siku tano ya Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya nje, Ulinzi na Usalama leo katika Ukumbi wa mikutano wa kimataifa JNICC Jijini Dar es Salaam.

Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Africa Mashariki Balozi Joseph Sokoine akizungumza wakati wa kufunga mafunzo ya siku tano ya Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya nje, Ulinzi na Usalama leo katika Ukumbi wa mikutano wa kimataifa JNICC Jijini Dar es Salaam.

Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama, Mhe.Musa Hassan Zungu akizungumza wakati wa kufunga mafunzo ya siku tano ya Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya nje, Ulinzi na Usalama leo katika Ukumbi wa mikutano wa kimataifa JNICC Jijini Dar es Salaam.

Waziri wa Ulinzi na Jeshi la kujenga Taifa Dkt. Stargomena Tax akiwapatia vyeti vya ushiriki wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje Ulinzi na Usalama mara baada ya kufunga mafunzo ya siku tano ya wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje Ulinzi na Usalama leo katika ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere JNICC Jijini Dar es Salaam.

Waziri wa Ulinzi na Jeshi la kujenga Taifa Dkt. Stargomena Tax akipata picha ya pamoja na wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje Ulinzi na Usalama mara baada ya kufunga mafunzo ya siku tano ya wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje Ulinzi na Usalama  leo katika ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere JNICC Jijini Dar es Salaam.

(PICHA ZOTE NA EMMANUEL MBATILO)

********************************

Waziri wa Ulinzi na Jeshi la kujenga Taifa Dkt. Stargomena Tax amesema serikali itahakikisha inatoa fursa ya mafunzo ya diplomasia ya mara kwa mara kwa Kamati ya bunge ya kudumu ya mambo ya nje Ulinzi na usalama ili kuimarisha maarifa ya wajumbe juu ya maswala mbalimbali ikiwemo uchumi.

Dkt. Tax ameyasema hayo mapema hii leo wakati akifunga mafunzo ya siku tano ya wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje Ulinzi na Usalama ambapo amesema Ulinzi na usalama haviwezi kutenganishwa na maswala ya kidiplomasia kwa kuwa ndio maslai ya taifa.

Ameongeza kuwa Kamati inalo jukumu la kuhimiza matumizi mazuri ya mitandao nanyenzo nyingine za teknolojia kwakuwa teknolojia isipotumika vyema itahatalisha usalama wa wataifa

Kwa upande wake Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Africa Mashariki Balozi Joseph Sokoine amesema mafunzo hayo yamelenga kusaidia kuwajengea uzoefu Katika maswala ya kidiplomasia ya uchumi, maslai ya Taifa, uchumi wa blue, na uhifadhi wa nyaraka za kibalozi.

Nae Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama, Mhe.Musa Hassan Zungu amesema taifa haiwezi kukwepa kushirikiana na wawekezaji wa nje kwani kuna miradi mikubwa inayoitaji utekelezaji wa baraka kwa kushirikiana nao itasaidia kupata teknolojia mpya na ubunifu.

“Uchumi imara. Inahitaji mabadiliko ya kidiplomasia hivyo watanzania tusiogope miradi mikubwa ambayo ndio chachu ya mabadiliko ya Taifa letu”. Amesema Mhe.Zungu.

Aidha ameushukuru Wizara hiyo kwa kuwapatia mafunzo hayo kwani itasaidia wawapo katika majukumu yao kutetea maslahi mapana ya Taifa.