Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Profesa Makame Mbarawa amesema mradi wa ujenzi wa barabara njia nane kutoka Kimara hadi Kibaha inayojengwa kwa gharama ya Sh bilioni 161 kulia ni Ofisa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara Tanzania (Tanroads) Rogatus Mativila.
Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Profesa Makame Mbarawa amesema mradi wa ujenzi wa barabara njia nane kutoka Kimara hadi Kibaha akiwa ameongozana na baadhi ya watendaji wa mradi huo.
Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Profesa Makame Mbarawa akitoa maagizo kwa watendaji wa mradi huo mradi wa ujenzi wa barabara njia nane kutoka Kimara hadi Kibaha
Muonekano wa kipande cha mbarabara hiyo eneo la Kibamba.
Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Profesa Makame Mbarawa akimsikiliza Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara Tanzania (Tanroads) Rogatus Mativila wakati alipotembelea mradi wa ujenzi wa barabara njia nane kutoka Kimara hadi Kibaha.
Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara Tanzania (Tanroads) Rogatus Mativila ak.imsikiliza Barakaeli Mmari Meneja Mradi. wa BRT katika eneo la Kituo cha Gerezani.
Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Profesa Makame Mbarawa akiangalia picha inayoonyesha Fly Over ya Chang’ombe jinsi itakavyokuwa mara baada ya kukamilika.
Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Profesa Makame Mbarawa akikagua ujenzi wa Fly Over ya Chang’ombe jijini Dar es salaam.
Mbunge wa jimbo la Mbagala Mh. Abdallah Chaulembo akielezea jambo kuhusu baadhi ya changamoto zinazotokana na ujenzi huo.
Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Profesa Makame Mbarawa amesema mradi wa ujenzi wa barabara njia nane kutoka Kimara hadi Kibaha inayojengwa kwa gharama ya Sh bilioni 161, umefikia asilimia 94 ambapo tayari mkandarasi ameshalipwa kiasi cha Shilingi bilioni 149.
Amesema kazi inaendelea vizuri na ni mambo madogo tu ndiyo yaliyobakia kukamilishwa kwa barabara hiyo ikiwemo kuweka barabara za mchepuo katika Kituo cha Mabasi cha Kimataifa cha Magufuli na barabara hizo kujengewa taa za kuongezea wananchi na magari na taa za barabarani.
Ameagiza mkandarasai wa barabara hiyo ya njia nane kuhakikisha anamaliza haraka kazi zilizobaki ili iweze kuzinduliwa na wananchi waanze kuitumia.
Akizungumzia mkakati wa utekelezaji wa ujenzi wa vituo vya abiria kwa ajili ya mradi wa mwendokasi kutoka Kimara hadi Kibaha na amegiza ifanyike tathmini ya kuboresha zaidi njia hiyo ya mabasi ya mwendokasi.
Meneja wa Mradi huo wa Mwendokasi Barakaeli Mmari amesema ujenzi wa mradi huo utajumuisha barabara za juu tatu za urefu wa mita 150 na upana wa mita 24 kila moja, vituo 29 vya abiria, Karakana na kituo cha Uendeshaji.
“Sababu za kuchelewa kwa mradi huu ni tatizo la menejimenti ya mradi ambao hata hivyo tayari imeondolewa na sasa kuna programu mpya imetengenezwa ambayo itahakikisha mradi huo unaisha rasmi mwakani,”. Amesema Barakaeli Mmari.
Ameongeza kuwa sababu za eneo la kilometa mbili kubomolewa na kurudiwa tena ujenzi wake ni baada ya kubainika kuwa mchanga uliotumika kwenye zege hiyo ulikuwa mchafu kwa kuchanganyika na udongo wa mfinyanzi.
Amesema sababu zake ni Zege halihitaji uchafu hata kidogo na kama ni mchanga ndio haufai kabisa inatakiwa lisiwe na vumbi wala udongo.
Ofisa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara Tanzania (Tanroads) Rogatus Mativila, alisema mradi huo umeongezwa muda wake wa kukamilika ambapo sasa utakamilika Machi, mwakani wakati ulitarajiwa uwe umekamilika mwaka huu.
ujenzi wa mradi huo uliofikia asilimia 29 kwa sasa utajengwa kwa sehemu mbili ya kwanza itagharimu kiasi cha Sh bilioni 217 na ya pili ambayo ni majengo itagharimu Shilingi bilioni 45.