Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi CCM taifa Ndugu Shaka Hamdu Shaka akizungunza na Wana CCM Nachingwea mkoani Lindi akiwa katika ziara ya kikazi pamoja na wajunbe wa sekretarieti ya CCM.
Wana CCM wilayani Nachingwea mkoani Lindi wakimpokea Katibu wa NEC itikadi na Uenezi CCM Taifa wakati alipowasili wilayani humor.
……………………………..
Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa Itikadi na Uenezi Shaka Hamdu Shaka amewaeleza viongozi na watendaji wote ndani ya chama na serikali kushughulika na changamoto za wananchi badala ya kukaa ofisini.
Shaka ameyasema hayo akiwa ziarani Wilayani Nachingwea Mkoani Lindi leo Septemba 15, 2021.
Pamoja na mambo mengine ziara hiyo imelenga kuhamasisha na kuimarisha uhai wa chama kuanzia ngazi ya shina, kuhimiza mahusiano ndani ya chama pamoja na serikali.
Shaka ameendelea kuwahakikishia wananchi kuwa CCM na serikali vipo salama na imara katika mikono ya Mwenyekiti na Rais mahiri wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan.
*”Hii ni kwa sababu katika muda mfupi serikali anayoiongoza imetoa mwelekeo wenye matumaini makubwa ya kuimarisha ustawi wa wananchi, uchumi wa nchi yetu, kuvutia uwekezaji zaidi, kuzalisha ajira kwa vijana na kuimarisha ulinzi na usalama wa mipaka ya Nchi yetu na raia wote.”* Amesema Shaka
Shaka amewataka viongozi na watendaji wote ndani ya serikali kuchapakazi kwani Chama, Rais Samia na wananchi wanataka matokeo yanayoonekana na yanayopimika kutoka kwenye utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya CCM 2020-2025.
Wakati huo huo Shaka ameilekeza Wizara ya Nishati kuhakikisha wanamaliza tatizo la kukatikakati kwa umeme linaloendelea maeneo mbalimbali nchini ikiwemo Wilaya ya Nachingwea.
Shaka pia amewataka wananchi kujitokeza kushiriki kikamilifu katika zoezi la sensa ya watu na makazi itakayofanyika mwaka 2022. Alihimiza serikali inatumia gharama kubwa kukamilisha zoezi hilo kwani taarifa zake zina umuhimu mkubwa katika kusukuma maendeleo ya nchi mbele zaidi hivyo ni muhimu kila mmoja kulishiriki.
Shaka yupo kwenye ziara ya Sekretarieti ya CCM Taifa iliyopo kwenye ziara mkoani Lindi ikiongozwa na Katibu Mkuu wa CCM Ndg Daniel Chongolo.