Mkuu wa wilaya ya Iringa Mohamed
Hassan Moyo akisisitiza jambo kwa wahudumu wa afya alipokuwa kwenye moja ya mikutano ya hadhara ambapo ameamua kufanya ziara kijiji kwa kijiji kusikiliza kero za wananchi wa wilaya hiyo
Wananchi wakimsikiliza mkuu wa wilaya ya Iringa Mohamed Hassan Moyo wakati akisisitiza jambo kwa wahudumu wa afya alipokuwa kwenye moja
ya mikutano ya hadhara ambapo ameamua kufanya ziara kijiji kwa kijiji
kusikiliza kero za wananchi wa wilaya hiyo
Wananchi wakimsikiliza mkuu wa wilaya ya Iringa Mohamed Hassan Moyo wakati akisisitiza jambo kwa wahudumu wa afya alipokuwa kwenye moja
ya mikutano ya hadhara ambapo ameamua kufanya ziara kijiji kwa kijiji
kusikiliza kero za wananchi wa wilaya hiyo
Na Fredy Mgunda,Iringa.
MKUU wa wilaya ya Iringa Mohamed
Hassan Moyo amewaonya wahudumu wa afya wanaokiuka agizo la serikali
linalowataka kutoa kipaumbele kwa wazee kutoa huduma za kiafya na kwamba tabia
hiyo haivumiliki na watakaobainika watachukuliwa hatua kali za kinidhamu.
Kauli hiyo imekuja mara baada
ya kupokea kero kwenye mikutano ya hadhara katika tarafa ya Kiponzero na Mlolo ambapo
baadhi ya wazee wamemlalamikia mkuu huyo wa wilaya kunyanyaswa na wahudumu wa
afya wa tarafa hizo.
Wakizungumza kwenye mikutano ya
hadhara wazee hao walisema kuwa serikali imewajali kwa kuwapatia kadi za
matibabu kwa wazee kwa lengo la kuwawezesha kupata huduma za kiafya bure lakini
hali inakuwa tofauti pale wanapokwenye kupata huduma hiyo kwenye vituo vya
afya,zahanati,hospitali za wilaya hadi hospitali ya Rufaa ya mkoani Iringa.
Wazee hao walisema kuwa kuwa
mara nyingi wamekuwa wakienda kutaka kupata huduma ya afya lakini wamekuwa
hawapati huduma inayostahili kama ambavyo serikali imekuwa ikisisitiza mara kwa
mara kuwa wazee wanapaswa kupewa kipaumbele katika huduma za kiafya.
Walimuomba mkuu wa wilaya ya
Iringa kuhakikisha kuwa anapeleka kilio chao kwa serikali kuu ili nao waweze
kuhudumiwa vizuri kama wananchi wengine wenye kipato kikubwa kwa kuwa
wamelitumikia taifa hili kwa miaka yao yote ya maisha.
Aidha wazee hao waliongeza kuwa
licha ya kuwa na kadi hizo bado kumekuwa na tatizo la kuzipata dawa ambazo
wanakuwa wanaziitaji wakati huo kulingana na magonjwa ambayo wanakabiliana nayo
badala yake wamekuwa wakielekezwa kwenda kununua dawa nje ya vituo vya afya.
Akijibia kero hizo za wazee
mkuu wa wilaya ya Iringa Mohamed Hassan Moyo alisema kuwa wazee wote wa wilaya
ya Iringa ambao wanaumri wa kuanzia miaka 60 wanatakiwa kupewa kadi za matibabu
za wazee kwa kuwa hiyo ni haki yao kwa muji wa sera za serikali ya awamu ya
sita.
Alisema kuwa wahudumu wa afya
wilaya ya Iringa wanatakiwa kuacha mara moja tabia ya kuwatolea lugha chafu
wazee wanapokwenda kupata huduma za kiafya bara yake wanatakiwa kuwahudumia
kama wanavyowahudumia wateja wengine wanaokwenda kupata huduma hiyo.
Moyo alisema kuwa akisikia wahudumu
wa sekta ya afya wanatoa lugha hizo chafu watachukuliwa hatua kali za kinidhamu
kwa lengo la kukomesha tatizo hilo ambalo linaonekama kuwa sugu katika wilaya
hiyo.
“Kila zama na kitabu chake mimi
sipo tayari kuona wazee hawa wakinyanyaswa bila sababu yoyote ile ya msingi wanapokwenda
kupata huduma za kiafya kwa kuwa serikali imeamua kuwadumumia kutokana na
mchango wao katika taifa hili hadi hapa lilipofika” alisema Moyo
Moyo amewaomba wananchi na
wazee wote wa wilaya ya Iringa kutoa taarifa kwake endapo watatolewa au
hawatahumiwa vizuri na watumishi wa sekta ya afya katika wilaya hiyo ili
kuondoa kero hiyo na kuboresha huduma kwa wateja ambao wanakuwa wanaenda kupata
huduma za afya.
Moyo alimazia kwa kusema kuwa
lengo la serikali ya awamu ya sita ni kuboresha sekta ya afya kwa wananchi wa
wilaya ya Iringa na Tanzania kwa ujumla hivyo haitaji tena kuona watumishi wa
sekta hiyo wakikwamisha juhudi za serikali.