Home Mchanganyiko DC MOYO: AMUOKOA BINTI ALIYEKUWA AKIBAKWA NA BABA YAKE KWA ZAIDI YA...

DC MOYO: AMUOKOA BINTI ALIYEKUWA AKIBAKWA NA BABA YAKE KWA ZAIDI YA MIAKA KUMI.

0

 
Mkuu wa wilaya ya Iringa Mohamed Hassan Moyo akiongea na wananchi wa kijiji cha Mgama kuhusiana na maswala ya ukatili wa kijinsia ambayo yanaendelea katika kijiji hicho

Mkuu wa wilaya ya Iringa Mohamed Hassan Moyo akiongea na wananchi wa kijiji cha Mgama kuhusiana na maswala ya ukatili wa kijinsia ambayo yanaendelea katika kijiji hicho
Mkuu wa wilaya ya Iringa Mohamed Hassan Moyo akiwa na kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya ya Iringa walipomtembelea binti ambaye amekuwa akibakwa na baba yake mzazi  kwa zaidi ya miaka kumi(10)

Na Fredy Mgunda,Iringa.

Mkuu wa wilaya ya Iringa Mohamed
Hassan Moyo amemuokoa mwanamke aliyekuwa akibakwa na baba yake kwa zaidi ya
miaka kumi katika kijiji cha Mgama kitongoji cha katenge B baada ya kupokea
taarifa ya kitendo hicho kutoka kwa wananchi wa kijiji hicho kwenye mkutano wa
hadhara wa kusikiliza kero za wananchi wa vijiji vya wilaya hiyo.

Akiwa kwenye mkutano wa hadhara
wa kusikiliza kero za wananchi wa katika kijiji Mgama ndipo lilipoibuka swala
hilo baada ya mwananchi kufikisha lalamiko hilo kwa njia ya barua kwa mkuu wa
wilaya juu ya tuhuma hizo kwenda kwa bwana Pancras Kiyeyeu ambaye ni baba ya mtoto
huyo.

Baada ya kupokea barua hiyo
mkuu wa wilaya kwa kushirikiana na kamati ya ulinzi na usalama walifunga safari
hadi kwenye nyumba ambayo bwana Pancras Kiyeyeu anaishi na kumkuta binti huyo
ambaye inaelezwa amekuwa akibakwa na baba yake.

Akizungumza mbele ya mkuu wa
wilaya pamoja na kamati ya ulinzi na usalama wa wilaya ya Iringa,binti huyo alikiri
kufanyiwa kitendo hicho na baba yake mara kwa mara kwa kutumia nguvu na maneno
ya kumtishia kumuua endapo ataongea kwa watu wengine.

Binti huyo alisema kuwa amekuwa
akibakwa mchana na usiku na baba yake kwa zaidi ya miaka kumi hadi kumpelekea
kupata ugojwa na kuanguka anguka(kifafa) na kusababisha kuathirika kisaikolojia
ambako kumepelekea kudhohofisha afya ya binti huyo.

Wakitoa ushuhuda huo baadhi ya
ndugu na majirani wa mzee Kiyeyeu walisema kuwa kumekuwa na taarifa hizo mara
kwa mara jambo lilopelekea kumpeleka mzazi huyo kwa mwenyekiti wa Kitongoji cha
Katenge B ambaye alifanikiwa kulimaliza kwa ngazi ya kifamilia ambapo ni kinyume
na sheria za nchi.

Walisema kuwa mzazi huyo
imekuwa tabia yake kwa miaka mingi kwa sababu kumekuwepo kwa malalamiko ya siku
nyingi lakini yamekuwa hayafanyiwe kazi na uongozi wa kitongoji cha Katenge B na
kusababisha mzee huyo kuwa huru na kuendelea kutenda vitendo hivyo kwa ndugu
zake na watoto wake.

Mara baada ya kusoma barua na
kupata maelezo ya binti aliyebakwa,majirani na ndugu zake wa mzee kiyeyeu,mkuu
wa wilaya ya Iringa Mohamed Hassan Moyo alisema kuwa kitendo cha unyanyasi wa
kijinsia alichofanyiwa binti huyo hakikubariki katika jamii yeyote hasa hasa
katika wilaya hiyo.

 Moyo alisema kuwa uzalilishaji aliofanyiwa
binti huyo haukubariki hata kidogo kutokana na wananchi wengi wa kitongoji
hicho kulifahamu jambo hilo na kuliacha bila kulichukulia hatua kali za
kisheria wakimuacha binti huyo kunyanyaswa kijinsia na baba yake.

Alisema kuwa ameliagiza jeshi
la polisi wilaya ya Iringa kuhakikisha watuhumiwa wote wanakamatwa ndani ya
masaa ishirini na nne (24) na kufikishwa mahakamani mara moja kwa kuwa ushahidi
kwa kiasi kikubwa umekamilika mara baada binti na majirani kukiri kutokea kwa
kitendo hicho.

Moyo alitoa onyo kali kwa
wazazi na wananchi ambao wanafanya vitendo hivyo watachukuliwa hatua kali za
kisheria

Mara
baada ya agizo la mkuu wa wilaya ya Iringa kwa jeshi la polisi wilaya ya Iringa,
Jeshi hilo limefanikiwa kuwatia mbaroni watu wawili akiwemo
Pancras Kiyeyeu 62 mkazi wa Kijiji Cha Mgama Wilayani humo kwa tuhuma za
kumbaka nakumtendea ukatili wa aina mbalimbali Binti yake anayesumbuliwa na
ugonjwa la kifafa uliodhohifisha Afya yake.

 

Mtuhumiwa mwingine ni Mendilad Kitime
mwenye umri wa miaka 44 ambaye ni mwenyekiti wa Kitongoji Cha Katenge B kilichopo
katika kata Hiyo akidaiwa kutochukua hatua za kisheria kwa kuficha uhalifu huo
hivyo akishiriki kuruhusu Binti huyo kuendelea kutendewa ukatili huo na baba
yake mzazi kinyume na sheria za nchi zinavyotaka.

 

Aidha
kulingana na hali ya afya ya binti huyo anayedaiwa kutendewa ukatili huo
kuonekana kudhohofika zaidi, mkuu wa Wilaya ya Iringa ameagiza uongozi wa kata
kumfikisha kwa wataalam wa afya ili afanyiwe uchunguzi na kupatiwa matibabu ya
haraka.