Na Mapuli Misalaba, Shinyanga
……..
Mtu mmoja amefariki dunia na wengine saba kujeruhiwa kufuatia ajali ya Gari aliyokuwa amepanda kuligonga trekta kwenye eneo la kijiji cha Ishinabulandi kata ya Samuye Barabara ya tinde-Tabora.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga kamishina msaidizi wa Polisi GEORGE KYANDO amesema ajali hiyo imetokea jana majira ya saa 2,30 usiku katika kijiji hicho ambapo gari hiyo aina ya HICE yenye namba za usajili t.470 DEL iliigonga trekta lenye namba t.623 CKY hali iliyosababisha kifo cha abiria huyo na majeruhi saba
Gari hiyo ambayo ni mali ya kampuni ya kisimbo and sons limited ilikuwa ikiendeshwa na Sudi Ntawigaya 25,mkazi wa Ibinzamata wakati trekta ilikuwa ikiendeshwa na na Shija Steven mkazi wa Ishinabulandi
Kamanda kyando amewataja majeruhi hao kuwa ni Shija Deus, Mohamed Juma, wote hao ni wakazi wa Ishinabulandi Venence Jonas mkazi wa Ndala, Maneno Charles mkazi wa Kitangili wengine ni Paulo Stephano ambaye hakufahamika mara moja makazi yake, Shabani Moharmed mkazi wa Majengo mapya pamoja na Josia Magabe mkazi wa Kitangili katika Manispaa ya Shinyanga
Chanzo cha ajari hiyo ni uzembe wa dereva wa HICE kutaka kuyapita magari mengine kwa mwendo hatarishi na kwamba jeshi la polisi linaendelea kumtafuta dereva huyo ambaye ametoroka baada ya kutokea kwa ajali hiyo