Balozi wa Marekani nchini Tanzania Donald Wright akizungumza katika kikao cha uwasilishaji wa utekelezaji wa miradi Miradi 115 ya kitafiti inayofanyiwa kazi huku tafiti 35 zikifadhiliwa na Serikali ya Marekani ambayo Balozi huyo ametembelea Chuo cha MUHAS.
Naibu Makamu Mkuu wa Chuo ( Taaluma, Tafiti na Ushauri) Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS) Prof. Appolinary Kamuhabwa akizungumza katika kikao hicho.
Profesa Karim Manji akiwasilisha moja ya mradi kuhusu lishe unaotekelezwa katika chuo hicho.
Mkurugenzi Mtendaji Taasisi ya Moyo Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) akitolea maelezo kuhusu iradi nayotekelezwa katika taasisi yake.
Picha mbalimbali zikionesha wataalamu mbalimbali wakishiriki katika kikao hicho.
Balozi wa Marekani nchini Tanzania Donald Wright akiwa katika picha ya pamoja na wakuu wa taasisi mbalimbali Muhimbili na Ocean Road.
……………………………………..
Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS) kimeendelea kujimaarisha katika kufanya tafiti mbalimbali za magonjwa na namna ya kupambana nayo.
Miradi 115 ya kitafiti imeendelea kufanyiwa kazi huku tafiti 35 zikifadhiliwa na Serikali ya Marekani ambapo leo Balozi wa Marekani nchini Tanzania Donald Wright ametembelea Chuo cha MUHAS.
Akizungumzia tafiti mbalimbali zinazofanywa ndani ya Chuo hicho Prof Bruno Sanguya amesema kuna miradi mingi inayoendelea kwa sasa ambapo serikali ya marekani kupitia NHI imeweza kufadhili miradi 35 yenye thamani ya Dola za kimarekani Milion 11 sawa na Bilioni 25 za Kitanzania.
Sanguya amesema Tanzania kupitia Chuo Kikuu cha MUHAS wameweza kushirikiana na serikali ya Marekanj kwa zaidi ya miaka 30 na imekuwa na mafanikio makubwa sana ikiwemo kuanzishwa kwa kliniki ya kwanza ya Kutoa dawa za kufubaza Virusi vya Ukimwi na ilikua ni ushirikiano wa MUHAS na Chuo Kikuu cha Havard.
Amesema, MUHAS wanaendelea kufanya tafiti hususani za magonjwa yasiyo ya kuambukizi ambayo yameongezeka kwa kasi na tafiti ni muhimu ili kufahamu namna ya kupambana nayo.
“Tumekuwa tunafanya tafiti hasa za magonjwa ya kuambukiza ila kwa sasa tunaendelea kujikita zaidi kwenye magonjwa yasiyo yakuambukiza kama Magonjwa ya moyo, saratani ambayo yameongezeka kwa kasi na hizi zinasaidia hata kwa watafiti wengine duniani katika kufahamu changamoto hizo,” amesema Sanguya
Kwa upande wa Tafiti juu ya Ugonjwa wa Uviko, Sanguya amesema waliweza kufanya tafiti ikiwemo namna ya kujikinga, kuvaa barakoa na hata aina za barakoa ambazo zinapitisha vijidudu na pia MuHAS tumeweza kuzalisha vitakasa mikono.
Balozi wa Marekani….ameishukuru serikali ya Tanzania na Chuo Kikuu cha MUHAS kwa kazi nzuri wanayoifanya na kuahidi kuendelea kushirikiana nao katika tafiti mbalimbali.
Amesema, Tanzania imekuwa na mchango mkubwa kwenye Kufanya tafiti zao na wameweza kuzituma kwa watafiti wengine duniani .
Marekani wameweza kufadhili Kuanzia miundo mbinu kwa kujenga maabara, kujenga data monitoring system, kuongeza uwezo kwa watafiti ikiwemo maadili ya tafit na maadili ya Kisayansi.
Balozi Wright amefanya ziara katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi (MUHAS), Taasisi ya Saratani ya Ocean Road (ORCI) na Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) ambako ameelezwa jinsi tafiti za kudhibiti magonjwa mbalimbali zilivyofanyika. Utafiti huo umejumuisha magonjwa ya afya ya akili, malaria, kifua kikuu, ajali na magonjwa yasioambukiza.