Benki ya NMB imekagua nia zitakazopitia mbio za NMB Marathon 2021 zinazotarajiwa kufanyika Oktoba 18 ,2021 zikianzia kwenye viwanja vya Readers Kinondoni jijini Dar es Salaam ambazo mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh. Kassim Majaliwa .
Akizungumza mara baada ya ukaguzi huo wa njia Bi. Jesca Sanga ambaye ni nahodha wa klabu ya NMB Jogging, amesema kwa kuwa muda wa kujiandikisha umeongezwa ili wadau na kujiandikisha kwa wingi ili wawe sehemu ya kuleta tabasamu kwa wanawake wenye Fistula.
“Lengo kuu la NMB Marathon 2021 ni kuwasaidia wanawake wenye changamoto ya ugonjwa wa Fistula, niwaombe wadau waendelee kujiandikisha ili wasaidie kuwapa tabasamu wenzetu wenye Fistula,”. Amesema Jesca.
Kwa upande wake, Bw. Othumani Amanzi, miongoni mwa viongozi wa Klabu ya Jogging ya Panja , amevishauri vilabu vingine kushiriki katika mbio hizo za NMB Marathon 2021 ili kushiriki katika harakati za kuchangia na kuwasaidia akina mama wenye ugonjwa wa Fistula.
Mbio hizo zitakazofanyika Septemba 25 mwaka huu, zitahusisha kilomita 5, 10 na 21 zenye kauli mbiu ya ‘Mwendo wa Upendo.