TAMASHA la Shukrani limepangwa kufanyika live huku wasanii mbali mbali wa muziki wa injili wakidhibitisha kushiriki tamasha hilo lililopangwa kufanyika Oktoba 31.
Wasanii waliodhibitisha Leo kutumbuiza kwenye tamasha hilo la kuombea taifa, na kumuombea Rais Samia Suluhu ni Martha Mwaipaja, Rose Muhando, na Martha Baraka
Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotion, Alex Msama, amesema wasanii hao wataungana na wenzao Upendo Nkone, Boniface Mwaitege, Jessica Honore, Messi Chengula pamoja na Enock Jonas kwenye kambi maalum ya mazoezi ambapo siku hiyo ya tamasha hakuna msanii atakaetumia CD au Flash na badala yake watatumia vyombo live.
“Hiyo siku licha ya kushukuru, tunataka watu waburudike,” alisema na kuongeza
“Mkumbuke taifa letu limepitia katika mambo mengi sana, kila mtanzania anafahamu kauli mbiu yetu ni ‘Tanzania ni nchi yetu, tuipende, tuilinde’ atuna budi kuipenda na kuilinda nchi yetu, tumshukuru Mungu kwa ajili ya taifa letu la Tanzania.” alisisitiza Msama
Aidha Msama amesema baada ya tamasha hilo kufanyika jijini Dar es Salaam, pia litafanyika katika mikoa mingine 10.