MKUU wa Mkoa wa Dodoma Anthony Mtaka,akipata maelezo ya ujenzi wa wa kiwanda kikubwa cha mbolea kutoka kampuni ya Itra Com Kutoka Burundi kutoka kwa Mwekezaji kutoka kampuni ya Itra Com Musafiri Dieudonne kinachojengwa katika eneo la Nala nje kidogo ya jiji la Dodoma,wakati wa ziara ya kukagua na kujionea Maendeleo ya ujenzi wa kiwanda hicho leo September 6,2021.
MKUU wa Mkoa wa Dodoma Anthony Mtaka,akiwa katika ziara ya kukagua ujenzi wa kiwanda kikubwa cha mbolea kutoka kampuni ya Itra Com Kutoka Burundi kinachojengwa katika eneo la Nala nje kidogo ya jiji la Dodoma leo September 6,2021.
Baadhi ya wananchi wanaofanyika kazi katika kiwanda hicho wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Anthony Mtaka,wakati wa ziara ya kukagua ujenzi wa kiwanda kikubwa cha mbolea kutoka kampuni ya Itra Com Kutoka Burundi kinachojengwa katika eneo la Nala nje kidogo ya jiji la Dodoma leo September 6,2021.
MKUU wa Mkoa wa Dodoma Anthony Mtaka,akizungumza na wananchi akiwa katika ziara ya kukagua ujenzi wa kiwanda kikubwa cha mbolea kutoka kampuni ya Itra Com Kutoka Burundi kinachojengwa katika eneo la Nala nje kidogo ya jiji la Dodoma leo September 6,2021.
Mkuu wa Wilaya ya Dodoma mjini Jabir Shekimweri,akizungumza wakati wa ziara ya kukagua ujenzi wa kiwanda kikubwa cha mbolea kutoka kampuni ya Itra Com Kutoka Burundi kinachojengwa katika eneo la Nala nje kidogo ya jiji la Dodoma leo September 6,2021.
Mbunge wa Jimbo la Dodoma Mjini (CCM) Mh. Anthony Mavunde,akizungumza wakati wa ziara ya kukagua ujenzi wa kiwanda kikubwa cha mbolea kutoka kampuni ya Itra Com Kutoka Burundi kinachojengwa katika eneo la Nala nje kidogo ya jiji la Dodoma leo September 6,2021.
Mstahiki Meya wa Jiji la Dodoma Prof. Davis Mwamfupe.,akizungumza wakati wa ziara ya kukagua ujenzi wa kiwanda kikubwa cha mbolea kutoka kampuni ya Itra Com Kutoka Burundi kinachojengwa katika eneo la Nala nje kidogo ya jiji la Dodoma leo September 6,2021.
MKUU wa Mkoa wa Dodoma Anthony Mtaka,akimsikiliza Meneja wa Kituo cha Uwekezaji Kanda ya Kati (TIC) Abubakari Ndwata wakati wa ziara ya kukagua ujenzi wa kiwanda kikubwa cha mbolea kutoka kampuni ya Itra Com Kutoka Burundi kinachojengwa katika eneo la Nala nje kidogo ya jiji la Dodoma leo September 6,2021.
MKUU wa Mkoa wa Dodoma Anthony Mtaka,akimsikiliza Mwekezaji kutoka kampuni ya Itra Com Musafiri Dieudonne wakati wa ziara ya kukagua ujenzi wa kiwanda kikubwa cha mbolea kutoka kampuni ya Itra Com Kutoka Burundi kinachojengwa katika eneo la Nala nje kidogo ya jiji la Dodoma leo September 6,2021.
Muwakilishi wa Intracom Tanzania, Bw.Samson Rubenga,akitoa shukrani kwa Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Anthony Mtaka mara baada ya ziara ya kukagua ujenzi wa kiwanda kikubwa cha mbolea kutoka kampuni ya Itra Com Kutoka Burundi kinachojengwa katika eneo la Nala nje kidogo ya jiji la Dodoma leo September 6,2021.
……………………………………………………………….
Na.Alex Sonna,Dodoma
MKUU wa Mkoa wa Dodoma Anthony Mtaka amesema,uongozi wa Mkoa umejipanga kuhakikisha kuwa unaondoa urasimu pamoja na kuboresha Mazingira rafiki na Salama ya kufanya uwekezaji.
Kauli hiyo ameitoa leo September 6,2021 jijini Domara baada ya kufanya ziara ya kutembelea Ujenzi wa kiwanda kikubwa cha mbolea kutoka kampuni ya Itra Com Kutoka Burundi kinachojengwa katika eneo la Nala nje kidogo ya jiji la Dodoma, Mtaka amesema lazima wahakikishe Urasimu wote unaondolewa ili kuwepo na mazingira bora ya kuwekeza.
“Tutakapoondoa urasimu tutapata wawekezaji na hawa watu watatusaidia kama hivi vijana wetu wanapata ajira lakini pamoja na kupata ajira muwajali wakiwa kazini muwape vitendea kazi na kauli nzuri wawapo kazini”amesema Mtaka
Aidha amekemea tabia ya wawekezaji kuondoa wafanyakazi wanaowasilisha mawazo yao na kutaja hatua hiyo kuwa haikubaliki katika sheria ya Tanzania,huku akiweka msisitizo kile alichokitaja kama ni Watanzania kupewa kipaumbele katika ajira na si watu wengine.
Mtaka ameutaka uongozi wa kampuni hiyo kuweka usawa katika kazi kwa wazawa kwani katika kiwanda hicho kumeonekana kuwepo na idadi kubwa ya Watu kutoka Burundi kuliko Tanzania.
Kwa upande wake Emmanuel Mavunde mfanyakazi katika kiwanda hicho amesema wanakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo kuwa na wasiwasi ya kufukuzwa kazi hasa pale wanapohoji jambo huku wakitupiwa kauli ambazo si rafiki na posho pia ni ndogo ikilinganishwa na kazi wanazo fanya.
Mwekezaji kutoka kampuni ya Itra Com Musafiri Dieudonne, ameiomba Serikali kuwatatulia changamoto ya kukatika kwa umeme, maji kutopanda, miundo mbinu ya barabara pamoja na usalama wao.
Kwa upande wake Muwakilishi wa Intracom Tanzania, Bw.Samson Rubenga amesema watahakikisha wanafanya kazi usiku na Mchana ili kuhakikisha kiwanda kinafikia lengo.
Hata hivyo kiwanda hicho kinatarajia kukamilika june 2022 ambapo kiwanda kitakuwa na uwezo wa kuzalisha mbolea tani laki 6 huku wananchi elfu 3 watapata ajira ya kudumu.