Home Mchanganyiko NHC YATEMBELEA UHONDO MEDIA JIJINI DODOMA

NHC YATEMBELEA UHONDO MEDIA JIJINI DODOMA

0

Viongozi wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) akiwemo Meneja wa Habari na Mahusiano Muungano Saguya pamoja na Afisa Habari Yahya Charahani, wametembelea makao makuu ya UHONDO MEDIA yaliyopo Jijini Dodoma na kupokelewa na Mkurugenzi wake Michael Msombe kwa lengo la kujadili namna bora ya kutangaza huduma zao kwa jamii ikiwemo miradi ya nyumba.

“Kama mnavyofahamu sasa hivi tunao mradi wa nyumba 1000 katika maeneo ya Chamwino Ikulu pamoja na Iyumbu, nyumba hizi zipo ambazo tunatarajia kuzipangisha na nyingine kuziuza kwa Wananchi tena kwa gharama nafuu kabisa kwa sababu lengo letu kuu ni kusaidia Jamii kila mmoja walau aweze kumiliki nyumba yake”- Muungano Saguya

“Nitoe wito kwa watanzania wakiwemo wakazi wa Dodoma kuichangamkia fursa hii adhimu ili kuweza kupata nyumba za kisasa kabisa kwa sababu uhitaji ni mkubwa na nyumba ni chache hivyo watu wakimbilie hiyo nafasi.”- Muungano Saguya

“Pamoja na hayo yote, nitoe wito sana kwa wale wapangaji ambao wanaishi kwenye nyumba za NHC kuendelea kulipa kodi zao kwa wakati ili basi kwa kutumia fedha hizo hizo sisi kama Shirika itatuwezesha kuongeza nguvu ya ujenzi wa nyumba nyingine nyingi kwa kasi ya uhitaji wa Wananchi na mwisho wa siku kila mtanzania aweze kumiliki nyumba yake kwa kupitia Shirika letu la NHC”- Muungano Saguya

“Tunawapongeza sana Uhondo Media ikiwemo Uhondo TV kwa kazi yenu nzuri ambapo mmekuwa mkishirikiana na sisi katika kuzitangaza shughuli za NHC na kiukweli tunakila sababu ya kuwashukuru kwakuwa mmekuwa mkifuata maadili yenu ya kazi na kujenga Imani kubwa kwa Jamii”- Muungano Saguya

Naye Afisa Habari wa NHC Yahya Charahani amesema “Uhondo TV mmekuwa mfano bora kwa namna mnavyokwenda na ni matumaini yetu kama NHC kwamba tutahakikisha tunashikamana bega kwa bega na kampuni yenu ili kuweza kufikia malengo”

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Uhondo Media, Michael Msombe amewashukuru NHC kwa kujenga ushirikiano nao pamoja na kuwaahidi kudumisha mahusiano yao ya kikazi, Msombe amesema>>>”Sisi kama uhondo Media tunawaahidi mazuri zaidi ya haya tunayoyafanya kwasababu tunaamini zaidi katika matokeo chanya ya kile tunachokizalisha”