RAIS wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania ,Askofu Gervas Nyaisonga,akizungumza wakati akifungua Mkutano Mkuu wa 84 wa mwaka wa Chama cha Madaktari wa Kikristo Tanzania (TCMA) uliofanyika leo September 6,2021 Jijini Dodoma.
Rais wa Chama cha Madaktari wa Kikristo Tanzania (TCMA) Dk.Bwire Chirangi akizungumza wakati wa ufunguzi wa mkutano mkuu wa 84 wa mwaka wa maaadaktari hao uliofanyika leo September 6,2021 Jijini Dodoma .
Baadhi ya washiriki wakifatilia hotuba ya Rais wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania ,Askofu Gervas Nyaisonga,(hayupo pichani) wakati akifungua Mkutano Mkuu wa 84 wa mwaka wa Chama cha Madaktari wa Kikristo Tanzania (TCMA) uliofanyika leo September 6,2021 Jijini Dodoma.
RAIS wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania ,Askofu Gervas Nyaisonga,akipokea kasha la tair la gari kwa ajili ya kupandika kwenye gari lake ujumbe uliopo katika kasha hilo mara baada ya kufungua Mkutano Mkuu wa 84 wa mwaka wa Chama cha Madaktari wa Kikristo Tanzania (TCMA) uliofanyika leo September 6,2021 Jijini Dodoma.
RAIS wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania ,Askofu Gervas Nyaisonga,akiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kufungua Mkutano Mkuu wa 84 wa mwaka wa Chama cha Madaktari wa Kikristo Tanzania (TCMA) uliofanyika leo September 6,2021 Jijini Dodoma.
……………………………………………………………………………..
Na.Alex Sonna,Dodoma
RAIS wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania ,Askofu Gervas Nyaisonga amewataka Madaktari nchini kuwa na huruma pamoja na kujiepusha na vitendo vya rushwa wakati wa kuwahudumia wagonjwa wanaofika kupata huduma za afya kwenye maeneo yao.
Kauli hiyo ameitoa leo September 6,2021 jijini Dodoma wakati akifungua Mkutano Mkuu wa 84 wa mwaka wa Chama cha Madaktari wa Kikristo Tanzania (TCMA),Askofu Nyaisonga amewataka Madaktari hao kuwa na huruma kwa wagonjwa na kuejiepusha na vitendo vya rushwa wakati wa kuwahudumia wagonjwa kwenye maeneo yao.
“Hapa juzi niliona clipu ya video na kuelezwa kuwa kunadaktari kamshona mgonjwa lakini inadaiwa kuwa baada ya kukosa fedha alimfumua huo mgonjwa,bahati nzuri sio wa hospitali zetu za diniya Kikristo,hivyo tuwe na huruma kwanza bila kujali masilahi ya fedha ”amesema Askofu Nyaisonga
Askofu Nyaisonga amesema kazi ya kuwahudumia wagonjwa ni ya wito,hivyo wanapaswa kufanyakazi kwa moyo wa kuthamini maisha ya binadamu na kujituma bila kushawishika au kuwa na tamaa ya kujinufaisha .
Amesema madaktari hao wamepewa dhamana ya kutunza afya za watu hivyo wanatakiwa kuzingatia maadili ya kazi yao na wajitume katika kuokoa maisha ya watu
Amewataka kujiepusha na mienendo inayochafua maadili ya udakitari na kuchafua Kanisa kwa sababu kazi zao inakiapo na ndani ya kiapo hicho huishi kusema Mungu anisaidie maana yake ni kazi muhimu sana kila siku .
Askofu Nyaisonga ameishukuru serikali kwa kuendelea kuruhusu na kushirikiana na mashirika ya dini zote nchini katika kuanzisha na kutoa huduma za kijamii hasa afya.
“Nawashukuru madaktari nchini kwa jinsi wanavyofanyakazi katika mazingira magumu hasa tangu ulipoingia ugonjwa wa homa ya Korona (UVIKO 19) pamoja na kukabiliwa na tatizo la rasilimali fedha lakini wamejitoa kuwasaidia wagonjwa,”amesema.
Amewataka madakitari hao kuwa viongozi wa Makanisa ya Kikristo Tanzania wataendelea kushirikiana na TCMA katika kuboresha huduma za afya kwa wananchi kwani taifa lisilokuwa na afya haliwezi kuwa imara na kupata maendeleo
Naye,Rais wa Chama cha Madaktari wa Kikristo Tanzania ,Dk Bwire Chirangi amesema mkutano huo wa 84 wa mwaka unajumuisha madaktari zaidi ya 300 kutoka vituo,zahanati na hospitali za makanisa yote nchini.
Amesema kuwa mashirika hayo ya dini yanachangia kwa kiwango kikubwa huduma za afya na ustawi wa jamii kuna hospitali 105 ambapo kati ya hizo 38 ni teule za Halmashauri na 10 zimepewa hadhi ya rufaa ya ngazi ya Mkoa .
Dk Chirangi amesema mashirika hayo yanamiliki zahati 720 na vituo vya afya 100 kote nchini na wanaendesha baadhi ya vyuo vya mafunzo ya wauuguzi na madaktari pamoja na vyuo vya kufundisha wataalamu wa ngazi mbalimbali.