Mkuu wa Wilaya ya Iringa Mohamed Moyo akijibu baadhi ya kero za wananchi wa tarafa ya Kiponzero alipokuwa kwenye ziara yake ya kusikiliza kero vijiji na mitaa yote ya wilaya hiyo
Mkuu wa Wilaya ya Iringa Mohamed Moyo akijibu baadhi ya kero za wananchi wa tarafa ya Kiponzero alipokuwa kwenye ziara yake ya kusikiliza kero vijiji na mitaa yote ya wilaya hiyo
Baadhi ya wananchi wa tarafa ya Kiponzero wakimsikiliza na kutoa kero zao kwa mkuu wa wilaya ya Iringa Mohamed Hassan Moyo
Baadhi ya wananchi wa tarafa ya Kiponzero wakimsikiliza na kutoa kero zao kwa mkuu wa wilaya ya Iringa Mohamed Hassan Moyo
Na Fredy Mgunda,Iringa.
Wanaume Wilayani Iringa yaiomba Serikali kuwanusuru na
vitendo vya ukatili wanavyotendewa na wake zao ikiwemo kupigwa na kudharirishwa
hali inayowaathiri kisaikolojia na kiuchumi vitendo wanavyovitaja kuchangia
baadhi yao kukimbia na kutelekeza familia kwa kuhofia usalama wao na aibu
katika jamii.
Wakizungumza katika Ziara ya kikazi ya Mkuu wa Wilaya ya
Iringa Mohamed Hassan Moyo yenye lengo la kubaini kero za wananchi na kuzipatia
ufumbuzi baadhi ya wanaume wa tarafa ya Kiponzero wamesema iko haja ya kuwapo
kwa dawati maaalum la utetezi wa haki za wanaume na usaidizi wa kisaikolojia
ili kuwaepusha na msongo wa mawazo kutokana na ukatili huo.
Miongoni mwa wanaume hao Walimueleza Mkuu wa Wilaya wake zao
wamekuwa na tabia ya kuwafanyia ukatili wa namna hiyo mara kwa mara lakini
jambo la kushangaza baadhi yao wanapotoa taarifa kwa viongozi wa Serikali za
vijiji na kata ili kupata usaidizi hawaoni hatua za moja kwa moja kuchukuliwa,
Alisema kuwa hatua inayosababisha baadhi yao kutafuta namna
za kukabiliana na ukatili huo hali inayopelekea kutenda uhalifu mkubwa zaidi
wakati wa kulipa kisasi na kusababisha kuongezeka kwa ukatili katika jamii.
Wanaume hao walisema kuwa baadhi yao wamekuwa wanashindwa
kutoa taarifa za vitendo hiyo vya unyanyasaji wa kijinsia kutokana na mila na
desturi za watanzania kuwa mwanaume kupigwa na mwanamke ni aibu kubwa katika
maisha.
“Kwa kweli sisi wanaume tunapigwa sana, yaani tunafanyiwa
vitendo vya ukatili wa kijinsia na tunashindwa kutoa Taarifa kutokana na mila
zetu sisi wahehe” walisema wanaume hao.
Aidha wanaume hao wameiomba serikali kuingilia kati kuhusu
vitendo hivyo kwani vimekithiri katika tarafa ya Kiponzero na kunasababisha
kuwanyima haki za msingi baadhi ya wanaume ambao wamekuwa wanafanyiwa vitendo
hivyo.
Akijibia changamoto ya Wanaume kupigwa kwa Niaba ya Mkuu wa
Jeshi la Polisi Wilaya ya Iringa (OCD), Afande Agustino Malema ambaye ni mkuu
wa Kituo cha Polisi Ifunda alisema kuwa jeshi la polisi limeanzisha kitengo cha
dawati la jinsia ambalo linahusika na matukio kama hayo.
Alisema kuwa hakuna mtanzania au mwananchi yeyote yule
anayetakiwa kufanyiwa vitendo vya ukatili wa kijinsi kwa kuwa mara nyingi
kitendo hicho kimekuwa kikiwaathiri kisaikolojia na kupunguza ufanisi wa akili
zao.
Afande Malema alisema kuwa wananchi wote wanaofanyiwa
vitendo hivyo wanatakiwa kutoa taarifa kwa jeshi la polisi bila aibu ili
kumaliza tatizo hilo ambao limekuwa linaibuka kwa kasi kwa kipindi cha miaka ya
hizi karibuni.
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Iringa Mohamed Moyo alisema
kuwa moja ya agenda yake katika ziara yake ni kutoa elimu ya kupinga
unyanyasaji wa kijinsia kwa wananchi wote wa wilaya hiyo ili kuondoka katika
nafasi waliyopo.
Moyo alisema kuwa mkoa wa Iringa na wilaya ya Iringa
vinaongoza kwa vitendo vya ukatili wa kijinsia hivyo ni lazima watafute njia ya
kukomesha vitendo hivyo ambavyo vinakuwa vikiharibu sifa kubwa ambayo wilaya
hiyo inayo.
Mkuu wa wilaya huyo aliwaagiza wenyeviti wa vijiji na
watendaji kuhakikisha wanavifichua vitendo hivyo vya ukatili wa kijinsia ili
kuwaondoa waathirika katika msongo wa mawazo ambao wanakumbana nao mara baada
ya kufanyiwa vitendo vya ukatili wa kijinsia
Alisema kuwa kitendo cha kumpiga mtu ni kosa la Jinai hata
kama amefanya kosa huku akiwataka wananchi wa kijiji hicho kwenda kuripoti
matukio hayo ya ukatili wa kijinsia katika vyombo vinavyohusika.