Home Michezo MWENYEKITI TWFA MWANZA  AFURAHISHWA NA MASHINDANO YA ANGELINE JIMBO CUP 2021.

MWENYEKITI TWFA MWANZA  AFURAHISHWA NA MASHINDANO YA ANGELINE JIMBO CUP 2021.

0
Mwenyekiti wa Chama Cha Soka la Wanawake Mkoa wa Mwanza TWFA Bi Sophia Makilagi amefurahishwa na uwepo wa mashindano ya mpira wa miguu Kwa Jimbo la Ilemela yanayojulikana kama Angeline Jimbo Cup 2021 yanayoendeshwa na Mbunge wa Jimbo la Ilemela Mhe Dkt Angeline Mabula akishirikiana na Chama Cha Mpira wa Miguu wilayani humo yanayohusisha timu kutoka kata zote 19 za wilaya ya Ilemela.
Akizungumza katika viwanja vya Shule ya msingi Sabasaba wakati wa mchezo wa robo fainali uliozikutanisha timu ya kata ya Ilemela dhidi ya timu ya kata ya Ibungilo Bi Sophia Makilagi amemshukuru na kumpongeza mwanzilishi wa mashindano hayo sanjari na kuwataka wachezaji kutumia fursa hiyo kwaajili ya kuonyesha vipaji vyao ili waweze kusajiliwa na mawakala wa vilabu vinavyoshiriki ligi mbalimbali 
‘.. Kiukweli nimefurahishwa na mashindano ya Angeline Jimbo Cup, Na nmefurahi kuona hatua hii ya robo fainali, Sisi wana michezo hatunaga maneno mengi lakini nawapongeza kikubwa yatumieni vizuri mashindano ..’ Alisema
Kwa upande wake Katibu wa Ofisi ya Mbunge wa Jimbo la Ilemela Mhe Dkt Angeline Mabula Ndugu Kazungu Safari Idebe amefafanua kuwa lengo la mashindano hayo ni kuibua vipaji vipya ndio maana wachezaji wanaoshiriki ligi hiyo si wale wanaoshiriki ligi Kuu, ligi daraja la kwanza wala ligi daraja la pili, Hivyo kuwaasa wananchi kujitokeza Kwa wingi kushuhudia hatua ya robo fainali ya mashindano hayo pamoja na kuziunga mkono timu zinazofanya vizuri
Akihitimisha Nahodha wa timu ya kata ya Ibungilo Damian Paul mbali na kushukuru Kwa timu yake kufuzu hatua ya nusu fainali amesema kuwa timu yake imepoteza nafasi mbalimbali za ushindi katika mchezo wa dakika tisini uwanjani hivyo kitendo  kilichotokea Cha kushinda Kwa hatua za mikwaju ya penati ni bahati na wanatakiwa kuongeza juhudi katika mchezo unaofuata Ili waweze kutetea ushindi wao walioupata katika msimu uliopita.
Timu ya kata ya Ibungilo iliishinda timu ya kata ya Ilemela Kwa mikwaju ya penati Tano Kwa tatu mara baada ya kutoka sare ya kufungana goli moja Kwa moja katika kipindi Cha dakika tisini za mchezo wa kawaida.