Kaimu Meneja Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) Mkoa wa Ilala Bw. Stephen Maganga, pia Afisa Usalama TANESCO Mkoa wa Ilala akizungumza na wakazi wa Kata ya Majohe leo jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kusikiliza kero zao, kuwapa elimu na kuwajengea uelewa namna wanavyotekeleza majumu yao pamoja na kutatua changamoto.
Afisa Uhusiano na Huduma kwa wateja TANESCO Mkoa wa Ilala Bw. Deusdedit Hokororo akizungumza na wakazi wa Kata ya Majohe leo jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kusikiliza kero zao, kuwapa elimu na kuwajengea uelewa namna wanavyotekeleza majumu yao pamoja na kutatua changamoto.
kushoto ni Afisa Uhusiano na Huduma kwa wateja TANESCO Mkoa wa Ilala Bw. Deusdedit Hokororo,Kaimu Meneja Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) Mkoa wa Ilala Bw. Stephen Maganga, pia Afisa Usalama TANESCO Mkoa wa Ilala , Mwenyekiti wa serikali za Mtaa wa Viwege Kata ya Majohe Bi. Amina Kapundi wakiandika kero na maoni ya wananchi wa Kata ya Majohe kuhusu utekelezaji wa huduma za umeme.
Afisa Uhusiano na Huduma kwa wateja Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) Wilaya ya Chanika Bi. Mwanaisha Mbita (upande wa kulia) akiandika namba ya mita ya umeme ya mteja baada ya kujibu swali kwa usahihi na kupatiwa zawadi ya unit za umeme.
Diwani wa Kata ya Majohe Bw. Mohamedi Ngonde akizungumza jambo katika kikao kati ya TANESCO Mkoa wa Ilala na wananchi wa Majohe.
Mwenyekiti wa serikali za Mtaa wa Viwege Kata ya Majohe Bi. Amina Kapundi akizungumza jambo katika kikao kati ya wananchi wa Mahoje na TANESCO ambacho kimelenga kusikiliza kero pamoja na kutatua changamoto mbalimbali katika kupata huduma ya umeme.
Mkazi wa Kata ya Majohe Bw. Denis Komba akiwasilisha kero kwa watendaji wa TANESCO Mkoa wa Ilala katika kikao kilichowakutanisha wananchi wote wa Majohe kwa ajili ya kupewa elimu na kutatua changamoto katika kupatiwa huduma za umeme.
Wananchi mbalimbali Kata ya Majohe wakiwa katika kikao na Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) Mkoa wa Ilala kwa ajili ya kusikiliza kero zao, kuwapa elimu na kuwajengea uelewa namna wanavyotekeleza majumu yao pamoja na kutatua changamoto.
……………………………………………………………………………..
NA NOEL RUKANUGA, DAR ES SALAAM.
Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) imewataka wananchi kuacha tabia ya kufanya shughuli za kimaendeleo karibu na miundombinu ya umeme ikiwemo transformer kutokana ina madhara makubwa endapo ikipata itirafu ambayo inayoweza kugharimu maisha ya watu wengi.
Maagizo hayo yametolewa TANESCO Mkoa wa Ilala wakati wakifanya kikao na wananchi wa Kata ya Majohe kwa ajili ya kusikiliza kero zao, kuwapa elimu na kuwajengea uelewa namna wanavyotekeleza majumu yao pamoja na kutatua changamoto.
Akizungumza na wakazi wa Kata ya Majohe leo jijini Dar es Salaam Kaimu Meneja Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) Mkoa wa Ilala Bw. Stephen Maganga, amesema kuwa hivi karibuni wataaza zoezi la kuwaondoa watu wote wanaofanya kazi zao karibu na transformer.
“Lazima tutawaondoa kwa nguvu watu wanaofanya kazi zao chini ya transformer kutokana inawahudumia watu wengi zaidi ya 200, hivyo ikitokea itirafu ya umeme madhara yake ni makubwa” amesema Bw. Maganga.
Bw. Maganga amesema kuwa utaratibu wa kulipa gharama za umeme ni sh. 27,000, hivyo amewata wananchi kutoa taarifa pale watakapo baini mfanyakazi wa TANESCO anaomba fedha kwa mteja kwa ajili ya kutoa huduma ya umeme.
Ameeleza kuwa mteja hatakiwi kuchangishwa gharama yoyote ambayo haipo katika utaratibu wa ofisi, kwani kufanya hivyo ni kuijuma serikali kutokana vitendo hivyo sio rafiki kwa mujibu wa taratibu za kazi.
Bw. Maganga ambaye pia ni Afisa Usalama TANESCO Mkoa wa Ilala, amewaomba wananchi kuendelea kutoa ushirikiano ikiwemo eneo la kuweka nguzo ya umeme pale itakapoitajika kulingana na mazingira husika.
Afisa Uhusiano na Huduma kwa wateja TANESCO Mkoa wa Ilala Bw. Deusdedit Hokororo, amefafanua kuwa kwa sasa kodi ya majengo inakatwa wakati unanunua umeme.
Amesema kuwa kuna changamoto ya baadhi ya wateja wana mita za umeme zaidi ya moja katika nyumba ambapo kwa utaratibu TANESCO hawana mamlaka ya kuamua lolote.
“Kama una mita ya umeme zaidi ya moja katika nyumba unatakiwa kwenda Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kutoa taarifa, na wao watatoa maelekezo TANESCO kuwa mita fulani msikate kodi ya majengo” amesema Bw. Hokororo.
Afisa Uhusiano na Huduma kwa wateja TANESCO Wilaya ya Chanika Bi. Mwanaisha Mbita, ameeleza kuwa kuna idadi kubwa ya watu wakipewa taarifa ambazo sio za kiofisi na kusababisha kutapeliwa na kuleta usumbufu.
Amesema kuwa taratibu rasmi za kupata huduma ya umeme wateja wanatakiwa kufika ofisi za TANESCO kwa ajili ya kupata fomu na maelezo.
“Nenda katika ofisi yoyote ambayo ipo karibu na wewe, hamtakiwi kumpa taarifa zako fundi, njoo mwenywe ufanye maombi ya kupata huduma ya umeme ili kuepuka usumbufu” Bi. Mbita.
Kwa upande wao wananchi wa Kata ya Majohe wameishukuru TANESCO kwa kuwapa elimu ambayo itawasaidia kuepukana na changamoto mbalimbali ikiwemo matapeli wakati wa kupata huduma ya umeme.