Home Mchanganyiko WAZIRI CHAMURIHO AWAHAKIKISHIA WAKAZI 644 WA MAGOMENI KOTA WOTE KUREJEA KATIKA NYUMBA...

WAZIRI CHAMURIHO AWAHAKIKISHIA WAKAZI 644 WA MAGOMENI KOTA WOTE KUREJEA KATIKA NYUMBA MPYA ZA KISASA 

0

Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Mhandisi Dkt. Leonard Chamuriho akizungumza na wakazi 644 waliokuwa wakiishi katika eneo lililojengwa nyumba za kisasa Magomeni kota leo Jijini Dar es Salaam.

Mtendaji Mkuu wa TBA Arch. Daud Kondoro akizungumza katika kikao cha Waziri Wa Ujenzi na Uchukuzi Mhandisi Dkt. Leonard Chamuriho na wakazi 644 waliokuwa wakiishi katika eneo lililojengwa nyumba za kisasa Magomeni kota leo Jijini Dar es Salaam. Wakazi 644 waliokuwa wakiishi katika eneo lililojengwa nyumba za kisasa Magomeni kota wakimsikiliza Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Mhandisi Dkt. Leonard Chamuriho alipokaa kikao na wakazi hao leo katika maeneo ya kota hizo leo Jijini Dar es Salaam.

(PICHA ZOTE NA EMMANUEL MBATILO)

**********************

WAZIRI Wa Ujenzi na Uchukuzi Mhandisi Dkt. Leonard Chamuriho amewahakikishia wakazi 644 waliokuwa wakiishi katika eneo lililojengwa nyumba za kisasa Magomeni kota kuwa, kaya zote zilizokuwa zikiishi hapo awali zitarejea katika nyumba hizo zilizojengwa kwa fedha za Serikali na kusimamiwa na Wakala wa Majengo Tanzania (TBA.).

Amesema wataishi katika nyumba hizo kwa miaka mitano bure kama ilivyoahidiwa na aliyekuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania Hayati Dkt. John Joseph Magufuli na sasa Serikali ya Rais Samia ambapo hajabadili ahadi hiyo.

Akizungumza na wananchi hao leo jijini Dar es Salaam, Waziri Chamuriho amesema, hadi kufikia mwezi Oktoba nyumba hizo zitakuwa zimekamilika na kaya zote 644 zitaingia katika makazi hayo mapya na kuwataka kupuuza habari zinazoenea zikieleza mabadiliko ya wakazi wapya wa maeneo hayo.

”Nyumba hizi ni kwa ajili ya kaya 644 kama ilivyoelekezwa na Rais, na kuna ongezeko na kaya 12 ambazo zitatumika kwa matumizi maalumu ikiwemo uongozi na utawala hivyo nitoe rai taarifa sahihi zinazotolewa na Serikali kuhusu makazi haya zinatolewa na Wizara na TBA na si vinginevyo hivyo, Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi inawatambua wakazi 644 watakaoingia na kuishi katika makazi haya.” Amesema.

Amesema kuwa baada ya wakazi hao kupeleka taarifa zao za uhakiki Wizara inaendelea na zoezi la uhakiki wa taarifa hizo na wategemee kuishi katika makazi hayo kwa mujibu wa ahadi ya Rais kwa kuishi katika makazi hayo kwa miaka mitano bure na watachangia gharama za huduma muhimu ikiwemo ulinzi, huduma jumuishi za usafi, maji, umeme na michezo ya watoto ambazo kwa sauti moja wakazi hao walikubali kuchangia huduma hizo muhimu.

Vilevile Waziri Chamuriho amesema miongozo na mikataba vinaandaliwa na watakabidhiwa siku ya kuingia katika makazi hayo na kuwataka kujiandaa kulinda mali ya Umma iliyojengwa kwa gharama kubwa na Serikali na kukamilika kwa asilimia 99 hasi sasa.

Akizungumza kwa niaba ya wakazi hao Bw.Semvua Ayoub amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kuwatumikia watanzania na kumwomba kuja kuzindua makazi hayo na kukabidhi funguo kwa mpangaji wa kwanza wa makazi hayo.