Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe Samia Suluhu Hassan aendelea na utekelezaji wa ufunguaji na ukuzaji wa uchumi wa Tanzania kwa
kutekekeleza miradi ya kimkakati kwa kasi ya ajabu.
Kufuatila ripoti ya Msemaji Mkuu wa Serikali (Habari Maelezo), Mhe. Gerson Msigwa amasema kuwa Serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Samia Suluhu Hassan imekwishalipa takribani shilingi bilioni 212.959 kwa ajili malipo ya awali ya ununuzi wa ndege nyingine tano. Pia Rais Samia ametoa Bilioni 50 kwa ajili ya ujenzi wa reli ya kasi (SGR) kuhakikisha mradi huo wa kimkakati unaendelea na kumalizika kwa wakati. Msigwa aliongeza kuwa Rais Samia pia katoa Bilioni 50 kwa ajili ya ujenzi wa mradi mkubwa wa kufua umeme wa Mwalimu Nyerere uliopo Mto Rufiji, Bilioni 20 kwa ajili ya utoaji elimu bure kwa watoto wa Kitazania na Bilioni 55.4 nyingine kwa ajili ya ujenzi wa Barabara.
Mbali na miradi hiyo ya kimkakati, *Rais Samia pia ametoa mabilioni ya fedha kutekeleza huduma za kijamii kama Umeme Vijijini (REA) na ununuzi wa nafaka.