******************
Nteghenjwa Hosseah, Dodoma
Waziri wa Nchi OR-TAMISEMI Mhe. Ummy Mwalimu amesema Serikali itajanga barabara ya Lami yenye urefu wa KM 13 ya Nzughuni- Mahomanyika Jijini Dodoma ili kuboresha mazingira ya Kata hiyo ambayo wananchi wamekua wakipata changamoto sana wakati wa mvua.
Waziri Ummy ameyasema hayo wakati wa ziara yake Jijini Dodoma kukagua ujenzi wa barabara za Mwangaza-Kisasa-Medeli, Nzughuni-Mahomanyika na ujenzi wa mifereji ya Mlimwa mapema leo Tar. 03.09.2021.
‘Nzughuni kuna idadi kubwa ya watu na eneo hili wakati wa Mvua linajaa maji hakupitiki lakini taarifa nlizopewa hapa ni kuwa fedha iliyotengwa ninya kujenga Barabara ya urefu wa KM 1.7 tu sasa nawaagiza TARURA waombe fedha za dharura kwa ajili ya kuweka lami barabara yote ya Nzughuni yenye urefu wa Km 13’ amesema Mhe. Ummy.
‘TARURA mnaweza kuanza kujenga Kwa awamu mkaanza na KM 5 kwa mwaka huu wa fedha kisha mkamalizia zingine mwaka unaofuata ila cha Msingo barabara hii yote iwekwe lami ili tuzidi kuboresha muonekano wa Makao Makuu Dodoma’ amesisitiza Mhe. Ummyz
Naye Mbunge wa Dodoma Mhe. Anthony Mavunde amemshkuru Waziri Ummy kwa kuskia kilio cha Wananchi wa Nzughuni na ameomba zaidi kuwa Daraja linalounganisha Nzuguni A na B ambalo limekua likileta maafa wakati wa mvua na changamoto kubwa kwa Wananchi liingizwe kwenye mpango wa ujenzi.
Waziri Ummy amehitimisha ziara yake kwa kuwaagoza TARURA waangalia namna wanavyoweza kuliingiza daraja hilo kwenye mpango mara ambapo ujenzi wa barabara hiyo ya Nzughuni- Mahomanyika utakapoanza.