Home Mchanganyiko DC IRINGA :WAZAZI WATAKAOWAOZESHA WATOTO KUKIONA CHA MTEMA KUNI

DC IRINGA :WAZAZI WATAKAOWAOZESHA WATOTO KUKIONA CHA MTEMA KUNI

0

Mkuu wa Wilaya ya Iringa Mohamed Hassan Moyo akigua mmoja ya shule za msingi zilizopo katika tarafa ya kiponzero ambapo kuna wanafunzi wa darasa la saba wanatarajia kuhitimu elimu ya msingi hivi karibuni
Mkuu wa Wilaya ya Iringa Mohamed Hassan Moyo akigua mmoja ya shule za msingi zilizopo katika tarafa ya kiponzero ambapo kuna wanafunzi wa darasa la saba wanatarajia kuhitimu elimu ya msingi hivi karibuni

Na Fredy Mgunda,Iringa.

Mkuu wa Wilaya ya Iringa ameonya kuwatia mbaroni na kuwafikisha Mahakamani
wazazi watakaobainika kuwashawishi watoto Wao kufeli kwa makusudi mitihani ya
kuhitimu darasa la Saba kwa lengo la kuwaozesha na ama kwenda kuwatumikisha
katika kazi za ndani nje ya Wilaya hiyo.

Akizungumza Kwenye ziara ya kusikiliza kero za Wananchi mkuu wa Wilaya hiyo
Mohamed Hassan Moyo alisema kuwa kumekuwa na tabia ya Wananchi kukatisha ndoto
za watoto kwa kuwashinikiza watoto wa kike kuolewa badala ya kuendelea na
masomo kutokana na tamaa ya fedha inayowakabili.

Moyo alisema kuwa wilaya ya Iringa imekuwa moja ya wilaya zinazoongoza kwa
ukatili wa kijinsia hasa dhidi ya watoto wa kike akiwataja wazazi ama walezi
kuwa sehemu watu wanaochochea kuongezeka kwa ukatili huo wakishitikiana na
baadhi ya viongozi wa vijijini kwa kuendelea kuficha uhalifu wanaotendewa
watoto hao wa kike.

Akiwa katika Ziara yake tarafa ya Kiponzero Mkuu wa Wilaya amewaagiza viongozi
wa vijiji na kata Wilayani humo kufanya sensa ya watoto watakaoanza mitihani ya
kuhitimu darasa la Saba  mwaka huu na kufuatilia mwendo wao Kabla na baada
ya kuhitimu lengo likiwa ni kupata Taarifa sahihi zinazowahusu Ili kuwalinda
wasiozeshwe ama kurubuniwa kwenda kufanya kazi za ndani katika maeneo
mbalimbali ya Miji.

Moyo alisema kuwa watoto wa
kike wanahaki ya kusoma na kuzifikia ndoto zao kama ilivyokuwa kwa wanawake
wengine wenye mafanikio makubwa dunia kwa kuwa walifanikiwa kuiishi ndoto yao
kutokana na wazazi kuwakuza kwenye malezi bora.

Wakiongea kwenye mikutano ya
hadhara inayongozwa na mkuu wa wilaya ya Iringa Mohamed Hassan Moyo wananchi
hao walisema kuwa kumekuwa na tabia ya wazazi kuwakatisha masomo kwa makusudi watoto
wao kwa tama ya fedha kidogo ambazo zimekuwa zikiua ndoto za watoto hao.

Walisema kuwa wameyasikia
maagizo ya mkuu wa wilaya hivyo watahakikisha wanafanya ulinzi shirikishi
kwenye vijiji vyao ili kuhakikisha kuwa wanakuwa na watoto ambao watakuwa huku
wakiishi kwa lengo la kutimiza malengo yao.