Katibu Mkuu wa wizara ya Madini, Prof Simon Msanjila akishuhudia wakati Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa STAMICO Dk. Venance Mwasse (wa kwanza kushoto) alipokuwa akibadilishana mkataba na Mkurugenzi wa Kampuni ya Buckreef, Khalaf Rashid kulia mara baada ya kusaini mkataba huo katika hafla iliyofanyika kwenye ofisi za Stamico Upanga jijini Dar es salaam leo.
Katibu Mkuu wa wizara ya Madini, Prof Simon Msanjila akishuhudia wakati Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa STAMICO Dk. Venance Mwasse (wa kwanza kushoto) na Mkurugenzi wa Kampuni ya Buckreef, Khalaf Rashid wakibadilishana yaraka za mktaba wa uchorongaji madini wenye thamani ya SH. bilioni nne.katika hafla iliyofanyika kwenye ofisi za Stamico Upanga jijini Dar es salaam leo.
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji STAMICO Dk. Venance Mwasse (wa kwanza kushoto) na Mkurugenzi wa Kampuni ya Buckreef, Khalaf Rashid wakionesha mkataba huo mara baada ya kuusaini katikati ni Katibu Mkuu wa wizara ya Madini, Prof Simon Msanjila.
Wageni Waalikwa katika hafla hiyo wakimsikiliza Katibu Mkuu wa wizara ya Madini, Prof Simon Msanjila wakati akizungumza.
Baadhi ya watendaji wa Kampuni ya Madini ya Serikali STAMICO wakiwa katika hafla hiyo.
………………………………………………
Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) limesaini mkataba wa uchorongaji na Mgodi wa Madini wa Buckreef (Buckreef Gold Company Ltd) ambayo ni kampuni inayochimba madini katika mkoa wa Geita.
Mkataba huo una thamani ya TZS bilioni nne na ni wa mwaka mmoja na kuna kuna uwekezano wa kuongezewa.
Akizungumza katika hafla ya kusaini kandarasi hiyo jana jijini Dar es Salaam, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji Dk. Venance Mwasse alisema mkataba huo utahusisha mitambo ya kisasa ya STAMICO ya uchorongaji ya Diamond Drilling (DD) na Reverse Circulation (RC) na uchorogaji wa awali utahusisha uchorogaji wa mita 10,000 za awali.
Alisema mradi huo unatarajiwa kuanza mwaka huu wa fedha 2021.
“STAMICO linamiliki mitambo mpya na ya kisasa ya uchorogaji ziadi ya minne yenye uwezo wa kutoa huduma ya uchorongaji kwa wateja wake kwa haraka zaidi na kwa viwango vya juu zaidi kiushindani.
“Kufuatia utiaji saini wa mkataba huo na kuanza kazi Shirika linatarajiwa kutoa ajira za muda mfupi kwa wakazi wazawa na kuchangia uchumi wa wilaya ya Geita na taifa kwa ujumla,” alisema.
“Tunaipogeza Kampuni ya Buckreef kupitia Mkurugezi Khalaf Rashid kwa kuiamini STAMICO kufanya kazi hii ya uchorongaji. “Shirika linaahidi kufanya kazi kwa bidii na uweledi mkubwa ili kutoa matokea yenye tija kwa kuwa ina mitambo ya kisasa na wataalamu wa kutosha.
“Shirika linatoa wito kwa wamiliki wa migodi na makampuni mengine nchini kutumia mitambo ya kisasa ya uchorongaji kutoka Shirika la madini la Taifa, kwani lina uwezo, wataalamu na vifaa vya kufanya kazi ya uchorogaji,” alisema.
Aidha, Mkurugenzi wa Kampuni ya Buckreef, Khalaf Rashid aliishukuru Stamico kwa kuendelea kushirikiana pamoja katika utekelezaji wa majukumu mbalimbali katika kuinua sekta ya madini nchini.
Wakati mgeni rasmi katika hafla hiyo, Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Prof. Simon Msanjilwa mbali na kuipongeza Stamico kwa miradi mbalimbali ya kimkakati iliyofanikiwa kuitekeleza, pia alilitaka Shirika hilo kuendelea kujiimarisha na kumiliki mgodi wake binafsi kwa asilimia 100 kwa siku za mbeleni.
Alisema mkataba huo uchorongaji ni mwendelezo wa kazi nzuri zinazofanywa na STAMICO kwani mwaka jana Shirika lilipata zabuni ya kuchoronga na kutafiti madini kutoka kampuni ya madini ya Geita Gold Mine Ltd. (GGML) wenye thamani ya Sh bilioni tisa.
“Ubora wa kazi zenu ndio unawafanya muendelee kupata zabuni nyingine kubwa na nzuri, Serikali tutaendelea kuwaunga mkono kwa sababu hata sasa utegemezi wa Stamico kwa serikali ni mdogo.
“Tutaendelea kuwaunga mkono hadi utegemezi uishe lakini pia kuhakikisha shirika linaendelea kutoa gawio kwa serikali kama mlivyoanza mwaka huu
“Shirika lilikuwa limekufa na lilitaka kufutwa kabisa lakini katika uongozi wa sasa ndani ya kipindi cha miaka mine mmefanikiwa kulifufua,” alisema.