****************************
Na Mwamvua Mwinyi,Kibaha
DIWANI wa viti Maalum Kibaha Mjini ,Lidya Mgaya amewaasa wanafunzi wilayani hapo ,kuachana na masuala ya utandawazi na kuiga mambo yasiyo na maadili na badala yake watumie TEHAMA kupata uelewa wa masuala mbalimbali ya kielimu.
Aidha amewaasa kusoma kwa bidii ili kujiinua kitaaluma .
Akigawa taulo za kike na sabuni za unga za kufulia kwa msaada kutoka KEDS TANZANIA COMPANY LIMITED na kisha kuwapatia baadhi ya wanafunzi wa shule ya sekondari ya wasichana Kibaha na Tumbi sekondari kwa wavulana, Lidya Mgaya alisema ,lengo ni kuongea na wanafunzi kutojihusisha na mahusiano ya kimapenzi na yasiyo na maadili wakati wanasoma.
Aliwasisitiza wasimame kuitafuta elimu kwa bidii na wafauru kusiwe na sifuri wala mimba za utotoni wakiwa wanasoma hivyo wajikite kuzingatia masomo na kuepuka mambo mabaya yatakayowarudisha nyuma kitaaluma.
Diwani huyo alielezea, amejipanga kuanza kampeni ya MWANAFUNZI WA KIKE KATAA MIMBA ZA UTOTONI KATAA ZERO hali itakayosaidia kupunguza changamoto ya kukatisha masomo kwasababu ya mimba, kufeli ama utoro.
Lidya aliishukuru halmashauri ya Mji wa Kibaha, ofisa elimu taaluma na sekondari pamoja na halmashauri na KEDs TANZANIA COMPANY LTD ambao wamemuunga mkono katika zoezi hilo la kupata taulo za kike.