Baadhi ya wafanyakazi wa benki ya NBC wakiokota takataka wakati wa zoezi la kufanya usafi wa mazingira kwenye ufukwe wa Msasani uliopo Mikocheni jijini Dar es Salaam hii leo. Zoezi hilo liliratibiwa na Klabu ya Rotary Dar es Salaam Peninsula na kudhaminiwa na wadau mbalimbali ikiwemo benki ya NBC.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NBC Bw Theobald Sabi akiokota takataka wakati wa zoezi la kufanya usafi wa mazingira kwenye ufukwe wa Msasani uliopo Mikocheni jijini Dar es Salaam hii leo. Zoezi hilo liliratibiwa na Klabu ya Rotary Dar es Salaam Peninsula na kudhaminiwa na wadau mbalimbali ikiwemo benki ya NBC.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Mkamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Selemani Jafo (Kushoto) akishirikiana na wadau mbalimbali akiwemo Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NBC Bw Theobald Sabi (Katikati) na Mwenyekiti wa Kamati ya Mazingira Taifa Bw Seif Ali Seif (Kulia) kufanya usafi wa mazingira kwenye ufukwe wa Msasani uliopo Mikocheni jijini Dar es Salaam hii leo. Zoezi hilo liliratibiwa na Klabu ya Rotary Dar es Salaam Peninsula na kudhaminiwa na wadau mbalimbali ikiwemo benki ya NBC.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki hiyo Bw Theobald Sabi (Katikati) akiwa kwenye picha ya pamoja na baadhi ya wafanyakazi wa benki hiyo mara baada ya kukamilisha zoezi la kufanya usafi wa mazingira kwenye ufukwe wa Msasani uliopo Mikocheni jijini Dar es Salaam hii leo. Zoezi hilo liliratibiwa na Klabu ya Rotary Dar es Salaam Peninsula na kudhaminiwa na wadau mbalimbali ikiwemo benki ya NBC.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Mkamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Selemani Jafo (wa tano Kushoto) akiwa kwenye picha ya pamoja na baadhi ya wafanyakazi wa benki ya NBC wakiongozwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki hiyo Bw Theobald Sabi (Kushoto kwake) mara baada ya kukamilisha zoezi la kufanya usafi wa mazingira kwenye ufukwe wa Msasani uliopo Mikocheni jijini Dar es Salaam hii leo. Zoezi hilo liliratibiwa na Klabu ya Rotary Dar es Salaam Peninsula na kudhaminiwa na wadau mbalimbali ikiwemo benki ya NBC.
………………………………………..
Dar es Salaam, Agosti 22,2021: Wafanyakazi wa Benki ya NBC wakiongozwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki hiyo Bw Theobald Sabi hii leo wameungana na Waziri wa Nchi Ofisi ya Mkamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Selemani Jafo, Klabu ya Rotary Dar es Salaam Peninsula pamoja na wakazi wengine wa jiji hilo katika kufanya usafi wa mazingira kwenye ufukwe wa Msasani uliopo Mikocheni jijini Dar es Salaam.
Akizungumza wakati wa zoezi hilo, Waziri Jafo pamoja na kuwapongeza wadau hao kwa jitihada hizo pia aliagiza Manispaa za Kinondoni, Ilala, Temeke na Kigamboni kuhakikisha zinatatua changamoto mbalimbali zinazokabili fukwe zilizopo kwenye manispaa hizo ikiwemo ukosefu wa vyoo.
“Suala la kuboresha huduma muhimu kwenye fukwe zetu si tu kwamba ni jukumu la Manispaa husika bali pia ni mojawapo ya chanzo cha mapato na ajira kwao. Manispaa zinapoboresha huduma hizi muhimu pia hata wananchi watajitokeza kwa wingi kwenye maeneo haya na pia watatumia huduma hizi kwa kuchangia kiasi cha fedha ambazo zitaongeza makusanyo kwa manispaa husika,’’ alisema.
Aidha Waziri Jafo aliongeza kuwa bado serikali hairidhishwi sana na usafi wa mazingira kwenye fukwe nyingi hususani jijini Dar es Salaam na jitihada za kukabiliana na changamoto hiyo zinaendelea kupitia watalaam pamoja na wadau mbalimbali wanaoshirikiana na serikali kutatua changamoto hiyo.
“Ndio maana nawapongeza sana Klabu ya Rotary kwa namna wanavyojitoa kushirikiana na serikali kutatua changamoto kama hizi kwa kushirikiana na wadau wengine kama vyuo vya elimu ya juu, makampuni binafsi na taasisi za kifedha ikiwemo benki ya NBC…huu ni mfano wa kuigwa hongereni sana,’’ alisema
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NBC, Theobald Sabi alisema ushiriki wa benki hiyo kwenye zoezi hilo muhimu ni muendelezo wa utaratibu wa kawaida wa benki hiyo kujitolea ama msaada au kushiriki moja kwa moja katika shughuli za kijamii ili kujenga ushirikiano kwa jamii wanayoihudumia.
Alisema fukwe hizo zinatumiwa na wananchi mbalimbali ambao pia ni wateja wa Benki hiyo hivyo wana kila sababu kusaidia kuboresha usafi wake ili kutoa fursa kwa watumiaji kupumzika katika mazingira safi na salama kwao.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Kamati ya Mazingira Taifa Bw Seif Ali Seif pamoja na kuipongeza serikali kwa namna inavyoshirikiana na wadau mbalimbali katika kuboresha hali ya mazingira nchini pia alitoa wito kwa jamii kwa ujumla kuhakikisha kwamba kila mmoja anakuwa askari wa kulinda usafi wa mazingira na uharibu wa miundombinu ya mazingira.
“Ni vema sana ikiwa jukumu la usafi wa mazingira likiwa shirikishi kwa maana ya kwamba kila mmoja wetu anakuwa mstari wa mbele kuhakikisha kwamba havumilii uchafuzi wowote utakaofanywa na mwenzie,’’ alishauri.
Awali akizungumza kwenye zoezi hilo Rais wa Klabu ya Rotary Dar es Salaam Peninsula Dr Edmund Issae ambae klabu yake ndio iliratibu zoezi hilo, alisema wamejipanga kuhakikisha washirikiana vema na wadau muhimu ikiwemo serikali ili kutatua changamoto zinazoikabili jamii ikiwemo suala zima la mazigira.
“Pamoja na kuwashukuru wadao wote waliotuunga mkono kufanikisha hili, nitoe wito kwao kwamba kwa pamoja tusichoke hadi tufike malengo yetu changamoto bado ni nyingi wadau zaidi wajitokeze,’’ alisema.